ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 11, 2013

Muda wa kubadili leseni za magari sasa waongezwa

Dar es Salaam. Matatizo ya kukatika kwa umeme ni miongoni mwa sababu zilizosababisha polisi nchini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kuongeza muda wa utoaji wa leseni mpya hadi Aprili 31 mwaka huu badala ya Machi 31 iliyopangwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema wamelazimika kuongeza siku baada ya kubaini kuwapo kwa mambo kadhaa yaliyokwaza baadhi ya madereva kubadilisha leseni zao kama inavyotakiwa.
“Tumebaini madereva hao walishindwa kubadili leseni zao kutokana na kukosekana kwa mtandao ambao ndiyo unawezesha mawasiliano ya kielektroniki kati ya TRA na trafiki, ingawa pia siku za kazi ziliingiliana na Sikukuu ya Pasaka’’ alisema.
Alisema baadhi ya madereva wengine nao hawajamaliza mafunzo yao ya PSV katika Vyuo vya NIT na Veta huku wengine wakichelewa kupewa vyeti vyao licha ya kumaliza mafunzo hayo,”alisema Mpinga.
Alisema kutokana na sababu hizo wameamua kuongeza muda ikiwa ni mwezi mmoja zaidi kuanzia Machi 31 ili madereva wachache waliobaki waweze kukamilisha taratibu za kubadilisha leseni zao, baada ya hapo hatutaongeza tena muda. “Hadi kufikia Aprili 8 ,leseni zipatazo 716,256 zilikuwa zimetolewa kwa nchi nzima, na kati ya hizo leseni 59,509 ni kundi lenye madaraja C na nyingine 656,749 ni za makundi mengine,” alisema Kamanda Mpinga.

Mwananchi

1 comment:

Anonymous said...

LICENCE? Seriously? Correction LICENSE!