ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 22, 2013

MWENDESHA BODA BODA ABIRIA WAKE WALIOKUWA MSAFARA WA LOWASSA IRINGA WAPATA AJALI

Dereva boda boda Japheth Aser akiwa na abiria wake Terresia Mapiu wakielekea eneo la Retco Bar ambapo walipata ajali mbaya ya boda boda kuhama njia na kutumbukia katika mtaro na kupelekea kujeruhiwa vibaya wakati wa ziara ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo mbaya iliyotokea wakati wa msafara wa Lowasa leo hapa ni baada ya boda boda hiyo kupata ajali katika mtaro ni boda boda yenye namba T 495 CCR

Dereva wa boda boda hiyo ambae ni majeruhi akiwa amepakiwa katika buti ya gari lenye namba T 910 CGA kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya ajali hiyo mbaya
Mmoja kati ya madereva boda boda ambae jina halikuweza kufahamika akisogea kutoa msaada kwa mwenzake aliyehifadhiwa katika buti ya gari baada ya ajali kutokea
Dereva boda boda akiwa hoi ndani ya buti ya Taxi akikimbizwa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa
Muuguzi Teresia Mapiu ambaye ni muumini wa kanisa la Overcomers POwer Center (OPC) mkoani Iringa akisubiri matibabu baada ya kupata ajali mbaya ya boda boda wakati akiwa kwenye msafara wa waziri mkuu mstaafu Edward LOwassa leo mjini Iringa
Hivi ndivyo muuguzi Teresia Mapiu alivyojeruhiwa katika ajali hiyo mbaya
Mmoja kati ya madereva bodaboda kushoto akiwa na muuguzi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa wakimsaidia dereva boda boda Japheth Aser aliyejeruhiwa katika ajali ya boda boda iliyotokea wakati wa msafara wa Lowassa
Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyombaya kwa kuitazama piki piki ikiwa katika mtaro eneo la Retco Bar  barabara ya Iringa -Dodoma mjini Iringa 
PICHA ZOTE NA FRANCIS GODWIN
MZEE WA MATUKIO DAIMA

No comments: