(6).jpg)
Mapitio ya Rufaa yaliyowasilishwa na makada watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Mahakama ya Rufaa kupinga ubunge wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema),Godbless Lema yanatarajiwa kuanza kusikilizwa Aprili 22, mwaka huu.
Kesi hiyo namba 21/2013 ilikatiwa rufaa na makada hao wa CCM Februari 13, mwaka huu chini ya hati ya dharura wakitaka yasikilizwe haraka.
Jopo la majaji kutoka Mhakama ya Rufaa wanaotarajiwa kufanya mapitio hayo ya rufaa ni jaji Nathalia Kimaro, Salum Massati na Bernard Luanda
Wanachama hao wa CCM, ambao ni Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, walifungua kesi dhidi ya Lema katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake, Lema alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Buriani.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment