ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 3, 2013

SAKATA LA KUGOMBEA KUCHINJA LAZUSHA BALAA TUNDUMA VURUGU TUPU

Mambo hayo 

Juu na chini Hii ndiyo hali halisi ya Mji mdogo wa Tunduma leo kuanzia asubuhi




Matairi yanachomwa katikati ya barabara

Diwani wa kata ya Tunduma Ndugu Frank Mwaijoka (Chadema) pamoja na mchungaji wa kanisa la KKT katika eneo hilo la Tunduma wilayani momba Mkoani mbeya wametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya kuhusika na uchochezi wa kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa vurugu katika eneo hilo.

Vurugu hizo zimeanza majira ya saa 3:asubuhi katika eneo hilo la tunduma mara baada ya kundi la watu wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo wakidai waruhusiwe kuchinja mifugo na kuuza katika mabucha yao hali iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.
Kwa picha na maelezo zaidi bofya read more
Akizungumza kuhusiana na tukio hilko Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi ya 40 tayari wamekwisha kamatwa .

Amesema mpaka sasa taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa miongoni mwa watu walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya Tunduma Ndugu John mwaijoka pamoja na Mchungaji wa kanisa la kkt ndugu Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja wametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Amesema suala hilo limegubikwa na siasa kwani tayari viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa huo Ndugu Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi Apri 02 mwaka huu wakiwepo pia viongozi wa dini .
Amesema kwa asilimia kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo ya kisiasa kwani hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika juu ya kutokea kwa vurugu hizo.

Amesema shughuli za kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika eneo hilo hivyo kufanya wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya Zambia ambao kwa asilimia kubwa wanategema kupata mahitaji kutoka mpakani mwa Tanzania.

Hata hivyo Diwani amesema kuwa katika vurugu hizo askari mmoja pamoja na mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe ambapo tayari wamekwisha fikishwa kituo cha polisi.

Kufuati hali hiyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kwa sasa hali imelejea katika hali yake ya kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu wakati jeshi hiulo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta wahalifu wengine.


Mwandishi wa Mbeya yetu pamoja na waandishi wenzake walipata shida sana kufika mji wa Tunduma walikutana na vikwazo vingi sana lakini wananchi walikuwa waelewa waliwasaidia kutoa magogo na matairi ili wapite wakapate habari

Mwandishi wa Mbeya yetu pamoja na waandishi wenzake walipata shida sana kufika mji wa Tunduma walikutana na vikwazo vingi sana lakini wananchi walikuwa waelewa waliwasaidia kutoa magogo na matairi ili wapite wakapate habari













































Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiongea na waandishi wa habari

Wanafunzi wakisindikizwa na jeshi la polisi kurudi majumbani mwao


Polisi wakiendelea kazi yao katika mitaa ya Tunduma



Baadhi ya magati ya IT yaendayo nchini Zambia yakiwa yamepakiwa nnje kidogo ya mji wa Tunduma kuogopa kuharibiwa kwa magari hayo


 
Picha na Mbeya yetu

3 comments:

Anonymous said...

cheki vitu na tasmini ewe muungwana mwenzangu mchangia mada katika blog hii, cheki picha hizi na picha walivyo kamatwa waislamu na polisi jinsi walivyo kuwa wakiwapiga kwa mabuti na kuwasonda ndani ya ndinga zao cheki halafu tuliza akili yako ujiulize hii kweli haki na kinachoendelea nini

janja janja zenu hizo

chinjeni nyama zenu nani kakukatazeni na msiwauziye waislamu muone kama watakufa na njaaaa

watu bwana wameshaamkaaa wako macho wazi usingizi wa pono umeshawatoka

kama siasa watu wanajua kama kusoma wameshasoma na kuelimika sasa hakuna cha ajabu ili kukutazameni action zenu mpo wakuuu

Anonymous said...

ebwana eeh nilidhani vita vya tatu ha ha ha kazi ipo kina waka juwa kali ha ha kisa udini ha ha ha mbona hawaifuati hiyo dini

Anonymous said...

SASA HAWA WALIOFANYA HIVI WANAITWAJE TENA? MBONA HAWAITWI WAHUNI AU AL KAIDA SHABAB BOKO HARAAM ETC TUAMBIYENI TUJUWE WANAITWAJE NA KWA NINI WAMECHUKUA HATUA MIKONONI MWAO

AU NDO DOUBLE STANDARD HIZOOOOOOOOOOOOOOOOOO KAZI IPO BONGO BONGO