ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 22, 2013

SERIKALI YA MUUNGANO HAIWANYIMI WAZANZIBARI MIKOPO

Naibu Waziri wa wizara, Zahra Ali Hamad
Na Salma Said
Zanzibar: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema si kweli kama Serikali ya Muungano inawanyima mikopo wanafunzi wa Zanzibar na kwa mwaka huu wananfunzi 237 wa Zanzibar wamepatiwa mikopo na aserikali ya Muungano.

Haya yalielezwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Zahra Ali Hamad wakati akijibu swali la msingi liloulizwa na Mwakilishi wa Wawi Saleh Nassor Juma wa CUF katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Alitaka kujua je ni lini serikali ya Muungano fedha za mkopo huo kwa upande wa Zanzibar zikatolewa katka fomula ya asilimia 4.5 kama vile Zanzibar inavyopata katika mambo mengine


Waziri alisaema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ni chombo cha Muungano kinachotoa mikopo kwa pande zote mbili za Jambhuri ya watu wa Tanzania ya kuwawezesha kujiuna na elimu ya juu.

Alisema ni kweli vigezo vya utoaji wa mikopo vya chombo hicho vinazingatia sifa ya muombaji, fani za kipaumbeale na hali ya umaskini wa familia ya mwanafunzi ambapo vigezo vya fani za kipaumbele na sifa za juu za waombaji zinatumika pia katika Bodi ya Mikopo ya Zanzibar.

Alisema kwa kutumia vigezo hivyo baadhi ya waombaji wa upande wa Zanzibar wamepata mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Tanzania Bara na badhi ya wanafunzi wanaokosa mikopo kupitia chombo hicho hupata kupitia Bodi ya Zanzibar.
Mwisho
Zanzibar: Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni, Jaku Hashim Ayoub ameuliza iwapo kima punju waliopo katika msitu wa Jonzani ni bora kuliko wanadamu wanaoishi maeneo ya Muungoni, Kitogani, Muyuni, Bwejuu na Pete.

Mwakilishi huyo aliuliza swali jana katika Baraza la Wawakilishi akitaka kujua ni kwanini barabara zinazopita maeneo hayo haziwekewi matuta ili kupunguza ajali wakati ile ya Jonzani ina matuta ili kuzuia kima wasigongwe na magari.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Mohammed Said Mohammed alisema serikali haina mpango wa kujenga matuta kwani hiyo sio njia sahihi ya kuzuia ajali.

Alisema suluhisho sahihi la kupunguza ajali barabarani ni kufuata sheria za usalama kwa watu wote wanaotumia barabara.

Alisema serikali itaendelea kutoa elimu ya usalama barabarani na idara zake ikiwemo ya Leseni itawachukulia hatua wote wanaovunja sheria hizo.

Mwisho

Zanzibar: Serikali ya Zanzibar imesema changamoto za ajira kwa watu wenye ulemavu ni nyingi kwa vile baadhi yao hawana sifa za kuajiriwa na wale wenye sifa hawaombi nafasi za kazi zinapotangazwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej aliyasema hayo jana katika Baraza la Wawakilishi wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Amaan, Fatma Mbarouk Said aliyetaka kujua ni walemavu wangapi wameajiriwa.

Mwakilishi hiyo pia alitaka kujua iwapo kuna mfuko maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kuweza kusoma kwa kuwapatia mikopo na ruzuku ili waweze kufikia malengo yao.

Waziri Fatma alisema suala la ajira si changamoto kwa walemavu tu bali ni kwa Wazanzibari wote.

Alisema Mfuko Maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu umeanzishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imeanzisha somo la Elimu Mjumuisho katika Chuo cha Kiislamu ili kutoa walimu wa kuwafundisha watu hao.
Mwisho

Zanzibar: Kila mfanyakazi anatakiwa kujua vifaa vya kuzimia moto vilipo na aweze kuvitumia ili kuzuia majanga sehemu za kazi.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirikia, Haruna Ali Suleiman aliyasema hayo jana katika Baraza la Wawakilishi nje kidogo ya mjini hapa.

Alikuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Amaan, Fatma Mbarouk Said aliyetaka kujua kuna vifaa vingapi vya kuzimia moto na juhudi zipi zimechukuliwa kuwafundisha wafanyakazi kukabiliana na ajali za moto.

Waziri alisema hatua iliyochukuliwa na wizara yake kupitia Idara ya Usalama na Afya Kazini ni kutea wawakilishi wa usalama kazini kwa kila wizara na mashirika ya serikali Unguja na Pemba.

Pia alisema kwa kujua umuhimu wa usalama kazini sheria zimeanzishwa zikiwemo za Usalama wa Afya Kazini namba 8 ya mwaka 2005, Utumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 2011 na Zimamoto na Uokozi ya mwaka 1999.

No comments: