ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 11, 2013

SMZ KUWANYANGANYA ARDHI VIGOGO

Na Salma Said, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itawanyanganya na kurudisha Serikalini ardhi itakayobainika kuchukuliwa na viongozi wa Serikali kinyume na utaratibu. Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Waziri wa Kilimo na Maliasili Ramadhan Abdalla Shaaban aliyekuwa akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni (CCM) Mbarouk Wadi Mussa aliyetaka kujuwa hatua zitakazochukuliwa kwa viongozi 'vigogo' waliojichukulia sehemu kubwa ya ardhi huko katika mashamba ya Serikali Selem Mkoa wa Kaskazini B Unguja.

Waziri Shaaban alisema yapo malalamiko makubwa wanaolalamikiwa viongozi kujichukuliya ardhi kubwa ya kilimo kiasi ya wananchi kuzusha malalamiko ikiwa pamoja na wawekezaji kulalalamikiwa.

“Sisi kama Serikali imeyasikia malalamiko hayo na inayafanyia kazi hata wewe Naibu Spika uliwahi kulalamika.....tukigunduwa kiongozi amechukuwa sehemu kubwa ya ardhi tutairudisha Serikalini na suala hilo

Shaaban alifafanua na kusema lengo la Serikali ni kuona wananchi wanapata sehemu ya ardhi kwa shughuli za kilimo kama ilivyofanywa awali na kiongozi wa Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume kwa kuwapatia wananchi eka tatu tatu za Kilimo.
Alisema wananchi wa kawaida wanatakiwa kupewa jumla ya eka tatu kwa ajili ya shughuli za kilimo, wakati viongozi wa Serikali watapewa jumla ya eka 10 kwani Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwa nia njema kabisa kwa kuwakomboa wananchi kutokana na unyonge wa kipato katika maisha iliamua kuwapa eka tatu kila mmoja.

Alisema wananchi wa Zanzibar walipatiwa eka tatu tatu kwa ajili ya kazi za kilimo na kutakiwa kuyaendeleza mashamba hayo kwa kazi hiyo ingawa wengi wao hivi sasa wametawaliwa na tama ya kuuza viwanja katika heka hizo.

Waziri Shaaban aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba kutokana na ardhi kuwa na bei kubwa. Hata hivyo katika shamba la Selem wengi wananchi waliokuwa wakilima hawakupewa heka tatu na serikali na ndio maana hawana hati rasmi ya mashamba hayo, isipokuwa waliingia kwa kulima tu, lakini bado mashamba hayo yanabaki kuwa ni ya serikali.

Akijibu sual la msingi la Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake Mwanaidi Kassim Mussa aliyeka akujua iwapo ni kweli kuna vigogo wamepewa eneo la Selem, Waziri huyo alisema.

“Ni kweli kuwa baadhi ya watumishi wa serikali wakiwemo waliostaafu waliomba nao wapatiwe ardhi ili wajiendeleze kimaisha kwa kazi ya kilimo hao pia ni wananchi wa nchi hii lakini hata hivyo hawakupewa sababu wao ni vigogo” alisema Waziri huyo.

Waziri huyo alisema wengi waliopewa ardhi walionesha mfano mzuri katika kuendeleza kilimo na kujipatia riziki ya kuendesha maisha yao.

Alifahamisha kuwa watumishi hao hawana tofauti na mkulima yoyote katika kuimarisha kilimo ambapo jumla ya ekari 139.0 zimetolewa kwa wananchi hao huko Selem.

Hata hivyo alisema suala la kuwapatia maeneo ya kulima wananchi wanaohitaji ardhi tayari suala hilo linafanyiwa kazi na Wizara hiyo kwa kuangalia maeneo matupu na kuyapima ili yaweze kugaiwa kwa wananchi hao japo kwa kiwango kidogo kama robo au nusu eka kwa kila mwananchi kwa vile maeneo yenyewe yaliyobaki ni madogo,

Sambamba na hayo Wwaziri Shaaban alisema suala la kuwa wananchi waliokuwa kwa muda mrefu na kuliendeleza shamba hili halikuwa sahihi kwa sababu wananchi hao walikuwa wakilima mazao ya chakula na sio mazao ya muda mrefu kama vile miti ya matunda au ya kibiashara.

No comments: