Nimeiona orodha ya nchi 20 masikini zaidi dunia na jambo la kufurahisha ni kuwa tanzania haipo kwenye orodha hiyo.nchi ya msumbiji ipo kwenye orodha ya nchi masikini lakini kuna jambo limenishangaza kidogo.thamani ya pesa ya msumbiji iko juu zaidi na ya kwetu kwa maana kwasasahivi 1000tsh = 18.97 meticais.sasa wale ndugu zangu wataalamu wa uchumi naomba mnisaidie kuhusu hili.kwa upeo wangu mdogo thamani ya pesa ya nchi fulani yaweza kutumika kama kigezo cha kubaini hali na kiwango cha uchumi wa nchi fulani?najua zipo sababu zingine kadhaa lakini hili limenishangaza kwa kiasi fulani
2 comments:
mnafuata orodha siku hizi ha ha ha, mbona bado mmelala usingizi wa pono ndugu zangu,angaliyeni jinsi wananchi wa hali ya chini wanavyoishi msijitape bure tanzania ni nchi maskini japo kuwa ni nchi iliyojaa kila madini mungu aliyoyabariki lakin mafisadi wanajinufaisha wao na ukoo wao na kuididimiza nchi hii so bado tupo maskin kwa mafisadi hawao
usisikiye politics is a dirty game
kukusaidia....curency haina uhusiano na umaskini. nchi yenye strong currecy duiniani ni nchi ndogo sana uarabuni-Kuwait ambapo 1 Kuwaiti dinar = 3.56125 U.S. dollars. Ila sio nchi yenye uchumi mkubwa duniani au tajiri sana duniani. Kigezo ni kuwa uchumi unaangaliwa kwa macho mengine na sometimes hayana ukweli wa kimaisha. Mfano, mtu anayeishi kijijini, mkulima na mfugaji, ana chakula, maji bure na labda anatumia umeme wa upepo au solar...je huyu anahitaji kuwa na pesa. Mimi namwita tajiri mkubwa maana anachakula fresh kila siku na anaishi maisha ya kweli. sasa hii haiangaliwi. utajiri unapimwa kwa gdp and awkward indicators.
Post a Comment