ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 17, 2013

Taswira Mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge Wakichangia Hoja Bungeni Mjini Dodoma

Spika wa Bunge Anne Makinda awaasa Wabunge kutumia Lugha ya Staha ambayo ni ya Kibunge wakati wa kuchangia mijadala Bungeni. Mhe. Makinda amesema, kuendelea kutumia lugha ya matusi, kejeli na maudhi kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ni kuendelea kuliondolea hadhi Bunge. 
Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola, akiomba Mwongozo kwa Spika Bungeni.
Mbunge wa Ukerewe Mhe. Salvatory Machemli akichangia Mjadala Bungeni .
Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Mhe. Kuruthum Mchuchuli akichangia kwa hisia mjadala Bungeni.
Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtembu akichangia Mjadala.
Waziri Mkuu Msaafu Mhe. Edward Lowasa akifuatilia kwa makini Mijadala Bungeni.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mhe. January Makamba akijibu baadhi ya hoja zilizochangiwa Bungeni .
Mhe. Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) akichangia Mjadala. Picha Zote na Picha na Ofisi ya Bunge

Pamoja na hilo, wabunge wanatakiwa kujikita katika kuchangia hoja zenye kutataua matatizo ya wananchi ili kutimiza wajibu wa kila mbunge wa kuwa wakilisha wananchi. 
Mhe. Makinda , amesema, fursa ya kila Mbunge kuchangia lazima ilenge kutatua matatizo ya wananchi na sio kutukanana na kusahahu jukumu lilomblele ya kila Mbunge. 
Katika Picha ni baadhi ya waheshimiwa Wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2013/14 Mjini Dodoma.

2 comments:

Anonymous said...

Why do those law makers seem to flex their uper body muscles and yale hile talking. Can't they just calm down, lelax and serve their energy for things like falling sky scrapers, form IV examinations' results, or after rain floods? Why can't they just stretch those micriphones to at least 180 degrees position, like what Makamba did, instead of bending to meet them down to their 90 degrees angle. Do we need foreighn assistance for this as well??????

Anonymous said...

Mchangiaji hapo juu, next time, tumia kiswahili kuchangia hoja zako, english language imekupitia kushoto kidogo....