Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi, Bw. Philippe Dongier kwa niaba ya Benki ya Dunia awaandalia chakula cha mchana watanzania waliohudhuria mikutano ya majira ya kipupwe mjini Washington DC.
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda Bw. Philippe Dongier pamoja na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa pia Gavana wa Banki kuu alikuwepo mwisho kulia.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Mchumi Mwandamizi wa Mkakati wa kupunguza umasikini Afrika Bw. Yutaka Yoshino pamoja na mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima wakibadilishana mawazo wakati wa chakula hicho.
Ujumbe wa Tanzania katika chakula cha pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania – Washington DC katika ofisi za ubalozi.
Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Harry Kitilya pamoja na Katibu wa Waziri wa Fedha Bw. Omary Khama wakati wa chakula cha pamoja.
jumbe wa Tanzania katika chakula cha pamoja. Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano Ubalozi wa Tanzania-Washington DC Bi Mindi Kasiga, Afisa Itifaki Wizara ya Fedha Bw. Cyprian Kuyava, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof. Longinus Rutasitara, watatu wanaofuata ni wachumi wa Wizara ya Fedha Bw. Erasto, Patric Pima, Veronica Maina na mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Dickson Lema.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Mdau wa Ubalozini Bw. Baraka Daudi na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha Bi. Eva Valerian wakitabasamu mara baada ya chakula cha pamoja katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Baadhi ya viongozi wa Tanzania waliohudhuria mikutano ya majira ya kipupwe katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania Washington DC. Waliokaa, kutoka kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Harry Kitilya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa Kaimu Balozi wa Tanzania Washington DC Bibi. Lily Munanka na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.
Ujumbe wa Tanzania katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania Washington DC aliyevaa blauzi nyekundu Bibi. Lily Munanka baada ya chakula cha pamoja.
Picha na Eva Valerian.
No comments:
Post a Comment