ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 13, 2013

Viongozi mbali mbali wamuenzi Waziri Mkuu wa Zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (mwenye tracksuti ya bluu),Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala (wa tano kulia) na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka,wakishiriki katika matembezi ya nusu kilomita ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kufariki kwa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,yaliyofanyika jana Apil 12, 2013 huko Kijijini kwao Monduli Juu,Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,aliefariki miaka 29 iliyopita.
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Wake wa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Mume wao.
Mbunge wa Jimbo la Arusha,Mh. Godbress Lema akishiriki mbio za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine zilizofanyika kijijini kwake Monduni Juu,Mkoani Arusha.
Baadhi ya vijana wa jamii ya Kimasai wakikimbia mbio fupi za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,kijijini kwake Monduli Juu,Mkoani Arusha. (LUKAZA)
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Telesphor Mkude akiwa na mapadre na waumini wakielekea eneo la kutolea maombezi ya kumbukumbu ya kifo cha Sokoine
Askofu Telesphor Mkude akiongoza sala ya maombezi ya kumwombea Marehemu Edward Sokoine baada ya kumalizika kwa ibada
Baadhi ya akina mama na watoto wao wakijumuika kanisani kumwombea Hayati Sokoine
kwa picha zaidi bofya read more
Hapa ndipo alipofia aliyekuwa Waziri Mkuu , Edward Moringe Sokoine , 
Aprili 12, 1984 akitokea Mkoani Dodoma. Eneo hili ni Wami Ruhindo , 
kilometa 40 kabla ya kufika mjini Morogoro
Baadhi ya kina mama wa Jamii ya wamaasai wa Kijiji cha Wami Sokoine ,
wilaya ya Mvomero wakiwa nje ya kanisa wakati wa ibada ya mumwombea 
marehemu Edward Sokoine
Kanisa laKatoliki Jimbo la Morogoro limejenga kanisa hili kumuenzi Hayati
Sokoine karibu na eneo alipopata ajali na kufariki dunia. Kanisa hilo 
linaitwa Picha ya Sokoine
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka (wa pili kutoka kushoto) 
na waumini wengine wakishiriki misa ya kumwombea Hayati Edward Sokoine eneo la Wami Sokoine.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ( kulia) akifurahia jambo na
Askofu , Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro eneo la 
Makao makuu ya Parokia ya Picha ya Sokoine

Jana Aprili 12, 2013 , Parokia ya Dakawa , wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro, ilifanya kumbukumbu ya Waziri Mkuu Hayati Marehemu Edward Moringe Sokoine kwa ibada ya misa takatifu iliyoendeshwa na Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, katika kanisa lilojengewa karibu na mahali alipofia baada ya kupata ajali ya gari Aprili 12, 1984 akitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam, sehemu alipofia hayato Sokoine ni Wami -Ruhindo,kilometa 40 kabla ya kufika mjini Morogoro na Kanisa alilojengewa na Jimbo Katolikila Morogoro linaitwa Kanisa la Picha ya Sokoine , tangu kufariki kwake dunia ametimiza miaka 29. Habari na picha na John Nditi.

No comments: