Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, mauaji hayo yalitokea juzi kati ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni.
Alisema marehemu alikutwa ameuawa kwa kukatwa shingoni kwa panga huku kichwa chake kikitenganishwa kiwiliwili.
Aidha, Kamanda Diwani alifafanua badaa ya mauaji hayo ya kikatili, muuaji huyo aliondoka na kichwa cha mtoto huyo.
Hata hivyo, alisema mtuhumiwa wa mauaji hayo alikamatwa na wananchi.
Kamanda Diwani alisema mtu hakufahamika jina lake lakini ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30 na 35.
Alisema baada ya wananchi hao kumkamata mtuhumiwa huyo, walimshambulia kwa fimbo na marungu.
Aidha, alisema wakati wananchi hao wakimshambulia kwa silaha hizo za jadi, walimbana mtuhumiwa aeleze mahali alikokipeleka kichwa cha mtoto huyo lakini alikataa kata kata.
Kamanda Diwani alisema hali hiyo iliwafanya wananchi wakasirike na kumteketeza kwa moto.
Hata hivyo, alisema chanzo cha mauaji ya mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Lusanje, kinahusishwa na imani za kishirikina na upelelezi wa polisi unaendelea sambamba na kukitafuta kichwa.
Wakati huo huo, mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina moja la Paul (60), amefariki dunia baada ya kugongwa na gari.
Kamanda Diwani alisema namba za usajili wa gari lililomgonga mtu huyo mkazi wa Ilemi jijini Mbeya, hazikufamika mara moja.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya. Aidha, alisema watu wawili wamekufa baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Tunduma.
Kamanda Diwani aliwataja watu hao ambao walikufa wakati wakipelekwa katika hospitali ya Ifisi kwa matibabu kuwa ni Side Ndasi (19) na Meshack Inkuru (24), wote wakazi wa Mbalizi jijini Mbeya.
Alisema gari lililowagonga watu hao ni lenye namba za usajili T516 AAA aina ya Toyota Chasser.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment