Hata hivyo, bado kocha wa timu hiyo, Mholanzi Ernie Brandts hakuwa tayari kusema ni nchi gani kikosi hicho kitakwenda kujifua kwa ajili ya michuano hiyo ya kila mwaka.
Brandts alisema kuwa kambi ya nje ya nchi husaidia kuwaimarisha wachezaji kimwili, kiakili na kuwaweka tayari kukabiliana na ushindani. Aliongeza kuwa wachezaji wanapokuwa nje ya nchi wanakuwa na wakati mzuri wa kufuatilia mafunzo na kuyafanyia kazi wanaporudi nchini.Alisema pia anafurahi kuona yuko katika wakati mzuri wa kuweza kutwaa taji la kwanza la ligi kuu akiwa na Yanga na la 23 kwa ujumla kwa klabu hiyo na anataka kuona pia wanatetea vyema ubingwa wao wa Kombe la Kagame.
Naye Afisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kikosi cha timu hiyo kitaingia kambini leo kujiandaa na mechi yao dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Mei Mosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kizuguto alisema wachezaji wote wanaingia kambini akiwamo beki Ladislaus Mbogo, ambaye alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa shavuni hivi karibuni.
Alisema kwamba wanataka kuona kikosi kinakuwa imara na kushinda mechi zao mbili zilizosalia dhidi ya Coastal na mahasimu Simba.
Vinara wa ligi kuu ya bara, Yanga, wanahitaji pointi moja tu kutwaa ubingwa na tayari wamejihakikishia moja ya nafasi mbili pekee za kushiriki michuano ya klabu barani Afrika.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment