Vijana wengi tumekuwa tukilalamika kwamba mabinti wa siku hizi wana mizinga ya reja reja ten mikubwa.
Ila hili jambo ukiliangalizia katika “big screen” ni jambo ambalo linakufanya utafute hela if you really want to be with a girl of your dreams though sio lazima a girl of your dreams awe mpiga mizinga!!!!! Jambo hili zuri nahisi vijana wengi hatujaligundua na badala yake tunalichukulia in a negative way na kubakia tunawalalamikia hawa mabinti, ila kumbe katika hali halisi wanatusaidia. Maana katika hali ya kawaida lets say kama umeajiriwa somewhere, mshahara peke yake hautoshi kumkeep huyo binti unayemuita wa kisasa au wa mizinga! Sasa kulingana na mahitaji yake kuwa makubwa lazima utatafuta njia nyingine za kupata hela tuseme labda utawekeza mahali. Lengo likiwa kuhimili mizinga ya huyo binti na kuendelea kumuweka karibu, ila mwisho wa siku unajikuta katika kuwekeza kwako una make faida zaidi ya hizo demands na kwa maana hiyo unakuwa na salio ambalo unaweza kujifanyia maendeleo yako mengine. Ila kama huyo binti asingekuwa na hizo demands kubwa ungeridhika na mshahara wako, maana utakuwa unawatosha na mwisho wa siku hata kuwekeza mahali huwezi fikiria , na maendeleo yako bila shaka yatakuwa si sawa na yule anayemmiliki binti wa kisasa!!!!!!!!!! Nahitimisha kwa kuwatia moyo mabinti wa kisasa waendelee na moyo wao huo huo wa kupiga mizinga tena mikubwa ili tutoke hapa tulipo kama Taifa!
2 comments:
nimekuelewa sana,mvivu ndio atachukia mizinga.
hapana mimi si kubaliani na hilo mabinti wa siku hizi pamoja na mizinga yao hawezi kuwa na mtu wa hali ya chini incase kama umelisahau hilo wengi wanakuwa na watu wazima ambao walishatengeneza maisha yao na familia zao na uwezo wao kifedha ni mkubwa,ama kama ni kijana basi awe ameshajijenga kimaisha na uwezo wao ni mkubwa na katika hapo hana mwanaume mmoja anawanaume kama watatu hivi kila mmoja na mzinga wake na mwisho wa siku anawatia loss na si faida kama unavyosema na ndio maana wengi wanalalamika kwasababu mwanamke huyu si wa future bali ni wa starehe, design ya mabinti hawa hupenda sana starehe na huwa hawapo mstari wa mbele kumshauri mwanaume huyo anaempiga mzinga kitu chochote,kwa hiyo kinachofuata pesa anayotafuta mwanaume yule ni kiasi kile kile cha kumstarehesha lakini si kwaajili ya maendeleo, nimeona mengi tu kupitia mabinti hawa
Post a Comment