Advertisements

Thursday, May 30, 2013

Fashion TV ya Ufaransa yaipa Runway Lounge Tuzo ya Kimataifa ya Night Life kwa kutoa huduma bora

IMG_0585
Mmiliki wa Runway Lounge iliyopo Shopper Plaza Samantar Abdinur Iusuf akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar akitokea Ufaransa ambapo amechaguliwa na Fashion TV Kuwa mshindi wa Tuzo moja wapo inayotambulika Kimataifa ya Night Life inayowakilisha huduma za kumbi za starehe (Night Club)katika nchi za bara la Afrika kama ilivyo Cavalli Club iliyopo Dubai, Cirque du Soir iliyopo jijini London na nyinginezo. Picha akiwa ameambatana na Mchumba ambaye pia ni mkewe mtarajiwa.
IMG_0587
Mmiliki wa Runway Lounge iliyopo Shoppers Plaza jijini Dar es Salaam Samantar Abdinur Iusuf akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa nchini Ufaransa.
IMG_0591
Mtoto wa kiume wa Mmiliki wa Club hiyo akifurahia mafanikio ya Baba yake baada ya kushinda tuzo yenye hadhi ya Kimataifa. Kushoto ni mchumba wake akiwa amembeba binti yake.
IMG_0599
Mmiliki wa Runway Lounge iliyopo Shoppers Plaza ya jijini Dar Samantar Abdinur Iusuf akizungumza na vyombo vya habari ambapo amesema Runway Lounge imekuwa ikendesha shughuli zake kwa muda wa miaka 5 iliyopita kwa mafanikio na kufanikisha Party mbalimbali zikiwemo Fashion Tv Parties na pamoja kuendesha party mbalimbali katika Hoteli ya Mediterraneo zinazofanyika katika fukwe za bahari ya Hindi na kutoa huduma zenye ubora wa Kimataifa.
Samantar ameongeza kuwa kwa kuwashukuru Watanzania na wageni mbalimbali tumamua kurudisha fadhila zetu kuanzia leo kuelekea kipindi hiki cha kiangazi (Summer time) Kiingilio kwa kila siku za Alhamis kitakuwa ni Shilingi 10,000 kwa usiku mzima na Kila siku ya Ijumaa na Jumamosi kiingilio kitakuwa Shilingi 15,000 mpaka saa tisa usiku na kwa kumalizia kutakuwa na Happy Hour kwa siku za Ijumaa na Jumamosi ambapo vinywaji vitauzwa kwa punguzo la 50% mpaka kufikia muda wa saa 8 usiku.
IMG_0607
Mmiliki wa Runway Lounge iliyopo Shoppers Plaza ya Mikocheni jijini Dar Samantar Abdinur Iusuf akionyesha moja ya koti la suti maalum lenye nembo ya Tuzo aliyoshinda kwa kutoa huduma bora za club.
IMG_0617
Oooh Give me a kiss Dad, Am Happy for your Success.....! Mmiliki wa Runway Lounge iliyopo Shoppers Plaza ya jijini Dar Samantar Abdinur Iusuf akishow love kwa binti yake.
IMG_0619
Mmoja wa waandishi wa habari akishow love na Mmiliki wa Runway Lounge iliyopo Shoppers ya jijini Dar Plaza Samantar Abdinur Iusuf mbele ya Camera ya Mo Blog.
IMG_0620
Brother from another Mother.....Zainul Mzige showing Appreciation to the Owner of Runway Lounge Samantar Abdinur Iusuf.
(Picha na dewjiblog).

No comments: