Sunday, May 26, 2013

Fedha Kessy na Nando waiwakilisha Tanzania kwenye Shindano la Big Brother-The Chase 2013


IMG_0156
Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini likitoa burudani wakati wa uzinduzi wa show ya Big Brother-The Chase iliyorushwa Live na Channel za DStv 197 na 198 jijini Johannesburg usiku huu. Shindano la Big Brother-The Chase limedhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. (Picha na Dewji Blog)
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari kutoka nchin mbalimbali za Afrika kushuhudia Live uzinduzi huo.
Mwakilishi kutoka Tanzania Ammy Nando akihojiwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Ik wakati wa uzinduzi wa show hiyo.Kushoto patna wa Nando Mshiriki kutoka Namibia Cleo.
Mwakilishi wa Tanzania Fedha Kessy akiwasalimu mashabiki wake kwa kuwapungia bendera ya Tanzania. Kulia ni mtangazaji wa Shindano la Big Brother The Chase 2013 Ik.
Mtangazaji IK akifanya mahojiano na Patna wa Mwakilishi wa Tanzania Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa Shindano la Big Brother The Chase lililozinduliwa rasmi leo jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo washiriki watakaa ndani ya jumba hilo kwa siku 90 na mshindi kujinyakulia kitita cha Usd 300,000. Kulia ni Fedha Kessy mshiriki kutoka Tanzania.
Mtangazaji IK akimtambulisha rasmi mshiriki kutoka Tanzania Fedha Kessy kwa Patna wake Mshiriki kutoka Ghana Elikem wakati wa uzinduzi wa shindano hilo leo jijini Johannesburg.
kwa picha zaidi bofya read more
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliopata mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa shindano hilo Live kutoka Kampuni ya Multichoice Africa. Wa pili kulia ni Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige aliyeiwakilisha Tanzania.
Kutoka kushoto ni Mwandishi wa habari kutoka Afrika Kusini Munya, Buhle na Thato kutoka Ofisi za Multichoice Afrika Kusini wakishow love back stage wakati wa uzinduzi wa shindano la Big Brother The Chase.
Wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali mbele ya camera yetu.
Mini Bar iliyondaliwa maalum kwa wageni waalikwa.
Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka nchini Kenya Stella Mwangi a.k.a STL akitoa burudani huku akipewa sapoti na Manager wake.
More pictures to come.

No comments: