Kibarua wa wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Iringa, Selemani Mbuma (pichani)mkazi wa Isoka mjini Iringa ambae alinasa katika nyaya za umeme wakati akiwa kazini baada ya wenzake kuwasha umeme afariki dunia leo
Kijana huyo alinasa katika umeme mwezi miwili iliyopita akiwa juu ya nyaya za umeme akiendelea na ufundi eneo la Mlandege kabla ya wenzake kuwasha umeme kimakosa wakati akiendelea na matengenezo na kupelekea kuungua vibaya mwilini .
Kijana Mbuma amefariki dunia mapema leo akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambako alikuwa akipatiwa matibabu na mwili wake unatarajiwa kuzikwa kesho .
Kifo cha kijana huyo kimeibua maswali mengi zaidi kutoka kwa vibarua wenzake na wamelitaka shirika hilo la Tanesco kuacha kuendelea kuwatumikisha vijana hao kwa maslahi duni ya chini ya Tsh.6000 kwa siku wakati kazi kubwa imekuwa ikifanywa na vibarua hao huku wafanyakazi ambao wanalipwa kila mwezi hukaa maofisini bila kazi.
Tanesco Iringa imekuwa ikilalamikiwa kutokana na tatizo la kunaswa kwa kibarua huyo katika nyanya za umeme na moja kati ya maswali ni pamoja na hili hivi hakuna hawawasiliani pindi wanapotaka kurudisha umeme huo? au hakuna fundi in charge ambaye ndio kiongozi wa msafara wa ufundi ambaye ndie atakaye husika na miongozo yote ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu anaye endelea na matengenezo ndio umeme uwashwe?
jibu naweza jipa mwenyewe kuwa lazima awepo ila ni Ufanyaji kazi wa mazoea na kuwaamini sana hawa wanaoitwa saidia kuwapa majukumu yaliyokuwa makubwa kuliko uwezo wao na ndio makosa kama haya yanatokea, maisha ya mtu yanapotea kwa uzembe wa kizembe kama huu.
Jambo jingine ambalo waweza kujiuliza kwanini fundi anafanya kazi bila kuvaa hata Grops mkononi wala mavazi ya kazi.
4 comments:
Very sad TZ yetu...hakuweza kuwa hata na helmet
Poleni wafiwa,nakumbuka ktk safari zangu ughaibuni,mavazi ya mafundi umeme huwa ni ya kitaalamu,sio nguo ya nyumbani kama picha ya huyo fundi. Je? Tz viwango vya utendaji kazi vikoje? Mbona tunautani?
Waliowasha umeme wachukuliwe hatua hakuna mjadala
Nikweli Tanzania tunautani na kifo kwanda marehemu kavaa sendozi jamani poleni sana wafiwa
Post a Comment