Na Mohamed Matope
Wakenya wengi walikuwa hawaijui International criminal court
( ICC), Koti ya Kimataifa mpaka wakati Raisi Uhuru Kenyatta na Makamu wake
William Ruto waliposhitakiwa. Vile vile wafrika
wengi wanaelewa kwamba watu wanaoshitakiwa kwenye koti ya kimataifa
ni viongozi wa nchi wanaotawala kwa mabavu na wauwaji wa raia wowote wanaowapinga
kisiasa kama, Charles Taylor wa Liberia au viongozi wa vita vya misituni vya kuipinga
serikali tawala (Warlords) kama Joseph
Kony wa Uganda .
ICC ni koti ya kimataifa iliundwa mwaka 2003, koti hii ina mamlaka
ya kuwahukumu watuhumiwa wa makosa ya mauwaji ya kipimo cha juu (genocide),
crimes against humanity na war crimes ndani ya Mtaifa yote yaliyosaini chata ya
Koti ya Kimataifa.
Cha kustaabisha ni kwamba, Raisi Kenyatta anashutumiwa na
ICC kwa kosa la crime agaist humanity, kwa kushiriki kwake kwenye mauwaji ya Wakenya baada
ya uchaguzi wa Raisi wa Kenya
wa mwaka 2007. Mashitaka ya Kenyatta kwenye koti ya kimataifa ni sawa na
mashitaka yanayomkabiri Joseph Kony wa Lord’s Resistance Army(LRA)
ya Uganda
na Bosco
Ntaganda kamanda Patriotic Force for the Liberation of the Congo (FPLC).
Wakenya wengi wanaomjua Kenyatta, hawajawahi kumuona amevaa
nguo za jeshi, au ameshika bunduki, au yuko msituni akiwa amezungukwa na vijana
wadogo wenye AK47 machine gun. Wakenya
wanamjua Kenyatta kama Mtoto wa baba wa taifa Jomo Kenyatta ,mfanyabiashara ,
mwanasiasa,mkikuyu na mtu anayeipenda Nchi yake.
Mauwaji ya Kenya ya mwaka 2007-2008, yalitokea baada ya uchaguzi
wa Raisi wa mwaka 2007, mauwaji hayo yalisababiswa na vita kati ya makabila ya
Wajaruo na Wakikuyu, pamoja na Wakikuyu na Wakalinjin.Vita hivi vilianza baada
ya mgombea uraisi Raila Odinga (mjaruo) alipokataa kukubaliana
na matokeo yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi ya Kenya, ambayo ilimtangaza Raisi Mwai Kibaki (Mkikuyu) kuwa mshindi wa
kura za Uraisi.
Ukweli wa mambo ni hivi, Kenyatta na Ruto hawakuwa wagombea
wa uraisi kwenye uchaguzi wa mwaka 2007.
Swali linakuja, kama Kenyatta na Ruto hawakugombea uraisi, kwanini wameshitakiwa kama
waanzilishi wa vurugu zilizofuata baada ya uchaguzi huo?
Vile vile watu wanajiuliza, kwanini kesi ya Kenyatta na Ruto
ilipelelezwa kwa kasi kubwa, na mashitaka yakaletwa mbele ya jaji wa mahakama ya kimataifa miezi
saba kabla ya uchaguzi mkuu? Kama ICC inaweza kuendesha kesi kwa kasi hivyo, mbona
haijamshitaki mtu yeyote kwa crime against humanity kuhusiana na vita vya Iraq na afganistani,ambapo maelfu ya raia
wameuwawa na vita vimekuwa vinaendelea
zaidi ya miaka kumi sasa?
Vilevile watu wanajiuliza hivi sasa imeshapita miaka miwili
tangu vita vya Syria
vianze na ICC bado inapeleleza tuhuma za war crimes katika mgogoro wa nchi hiyo,
kwanini inachukuwa muda mrefu kuwaleta watuhumiwa kizimbani? ICC ipo wapi
kwenye vita vya Israel
na Palestina? Au Migogo ya Ulaya ya
Mashariki?
Pamoja na hayo vile vile watu wengi
wanahituhumu koti ya kimataifa
kuwa ni fimbo ambayo Mataifa ya
Magharibi wanaitumia kuwachapa viongozi wa
Afrika. Kwa mfano toka ICC ianzishwe, miaka kumi ililiyopita
imeshatangaza watuhumiwa 32,ambao wote
ni Waafrika, kwa maana hiyo viongozi wa Afrika ndio watu pekee wanaouwa watu
kwa scale kubwa hapa duniani?
Kwa ufupi kesi ya Raisi Kenyatta haina miguu ya kusimama
yenyewe, kesi ililetwa Mahakamani kutokana na mashahidi ambao wanasema
walimsikia Raisi Kenyatta akiongea kuhusu kuwaajiri Mongiki (kikundi cha
uterolisti cha Kenya )
ili wawavamie kabila la Wakalenjin. Kati ya mashahidi hao shahidi mmoja tuu
(shahidi numba 5) ndiye aliyetestifai kwamba kama
alikuwepo wakati Raisi Kenyatta alipokuwa anawaajiri Mongiki.Na shahidi huyo
ametolewa katika kesi hiyo kwa sababu za rushwa na uongo.
Kwa kifupi ICC imechemsha kwenye uchaguzi wa Kenya,kwanza kwa
kuleta mashitaka ya Raisi Kenyatta na makamu wake William Ruto katika kipindi
ambacho siasa ilikuwa imechachamaa
nchini Kenya, katika kipindi cha uchaguzi mkuu.Kwani watu wote tunaelewa
jambo lolote linalokuja wakati wa uchaguzi lazima liwe na siasa ndani yake.
Pili , Kwa kawaida
kabla kesi haijafunguliwa, Mwendesha mashitaka anapeleleza kesi kuona uzito
wake na kukagua sehemu mauwaji yalipotokea (crime scene) kabla hajaipeleka kesi
mahakamani. Kwenye kesi ya Raisi
Kenyatta ilikuwa ni kinyume. Luis Gabriel Moreno Ocampo, mwendesha mashitaka wa ICC
aliifungua kesi ya Raisi Kenyatta na washitakiwa wengine kutokana na ripoti zilizo wasilishwa kwake. ICC haukutuma
Waendesha mashitaka wake nchini Kenya kuchunguza mauwaji ,kuongea na mashahidi,
kuongea na waathirika wa pande zote kabla haijaifungua kesi, na hilo lilikuwa
kosa kubwa sana kwa upande wa ICC.
Lakini kwa kuwa Koti ya Kimataifa ilishindwa kufauata hivi
vipengele viwili,koti hiyo imejikuta ikiingizwa kwenye uchaguzi kama chombo cha
kampeni na kupigwa kama mpira wa miguu na
matokeo yake imepoteza heshima yake yote ndani ya Bara la Afrika.
6 comments:
Mwandishi ,kweli kuna ukweli ,Kenyatta sio mtu wa msituni ,ICC ikopale ili kuidharilisha Africa ,vile vile umesahau kuongeza kwamba ICC imeshawashitaki Maraisi wawili tu ambao wapo madarakani,na Maraisi hao wote ni Waafrika.Sasa haki iko wapi? mwansishi mzuri sana hongera.
Bwana wewe acha visa vyako,hiki kitu kimekubali mno,tunataka waafrika kama wewe wanaotufunua mawazo,hii ni injustice kwa Afrika,kwanini sisi ndio washitakiwa kila siku,wakati Drone za USA zinaua innocent civilians huko Pakistan na Afganistan kama utitili.NATO imeshaua maelfu ya akinamama na watoto huko Afganistan .Kwanini hawashtakiwi.
Sasa ICC watafanyaje Kenyatta ameshachaguliwa uraisi,na mtu wao waliomtaka Raila Odinga ameshindwa ,sasa wamshitaki Odinga kwa kushindwa uraisi.Ili watoe fundisho kwa Waafrika kwamba musipomchagua mtu wetu sisi tutamfunga.
Bwana Matope ebu tueleze wewe mwenzetu Mkenya au Mbongo,maana haya mambo ya Kenya unavyoyaelezea kame wewe mzaliwa wa Kakamega.Kiukweli ni kwamba ICC ni vibaraka ,mimi nashangaa kwanini Nchi za Africa zilisaini nao mkataba .Hawa watu wanataka kuurudisha ukoloni tena Africa .Nasi hatutawakubalia.
Kama Ocampo alikuwa hana evidensi zozote basi alikuwa mjinga kuileta kesi mahakamani.Sasa unajua kwamba watu wawili walioshitakiwa na Kenyatta wameachiwa kwa kukosekana ushahidi?trust me its just a matter of time Kenyatta naye ataachiwa.
Mr this is certain true but i will like to suggest one thing ,i have been following your articles and i like them ,im Kenyan and i like your analysis of Kenyan election ,but you know some of us we are not that good in swahili.kiswahili yetu inaleta matata kidogo,so its best for you to continues to write us in English thanks.
Post a Comment