Monday, May 27, 2013

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NA KUMPA POLE KUFUATIA VIFO VYA ASKARI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo Mei 27, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo Mei 27, 2013. Picha na OMR
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

TAREHE 27, 2013

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na Mkuu wa jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Mei 27, 2013. 

Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais ametumia nafasi hiyo kumpa pole Mkuu wa Polisi kufuatia ajali ya gari la iliyosababisha vifo vya askari wanne wa Jeshi hilo, waliokuwa njiani kutoka Nachingwea kuelekea Mkoani Mtwara kwa kazi maalum ya kudhibiti vurugu zilizojitokeza Mkoani humo juma lililopita.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema, askari hao watazidi kukumbukwa kwa kuwa walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha majukumu yao kwa Taifa hili yanafanikiwa. Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema pia kuwa, serikali inathamini sana mchango wa Jeshi la Polisi sambamba na majeshi mengine kutokana na kufanya kazi kwa kujitolea na kwa kutambua kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Mkuu wa Polisi kuwa, kazi inayofanywa na jeshi lake ni kubwa na kwamba Watanzania wanaithamini sana. Pia aliongeza kuwa katika nchi zote wananchi wanaojitolea kufanya kazi katika vyombo vya usalama, ni miongoni mwa wazalendo wakubwa wanaopaswa kuenziwa kwa kuwa wamekubali kuweka maisha yao kwa ajili ya nchi na watu wake.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kupata taarifa kuhusu hali ya usalama mkoani Mtwara na pia kubadilishana mawazo kuhusu kuhakikisha maeneo ya nchi yetu kubakia salama wakati wote. 

Imetolewa na Boniphace Makene
           Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais

2 comments:

Anonymous said...

serikali yetu ya Tanzania inapaswa kuelewa kwamba wakati sasa umebadilika, hizi ni zama zinazotawaliwa na uwazi na utandawazi. masuala kama haya yanapaswa kujadiliwa na kutolewa maamuzi ya makini na busara kubwa. maguvu tu hayataendesha nchi bali itaipelekea nchi pahali pabaya. popote uendapo dunia hii iwapo itatokea sehemu kuna rasilimali basi ni lazima hiyo sehemu kwa njia moja ama nyengine ifaidike kwa angalau basi kuiendeleza kiuchumi, huduma za afya na elimu nk. tuwaangalie wanaigeria inachekesha na kusikitisha kuona hilo eneo la delta linalotoa mafuta kwa wingi ndilo halitamaniki kwa uchafu wa mazingira, umaskini uliokithiri na ubovu wa miundo mbinu. na angalia mfano wa usa kule Alaska wananchi wanapofanya tax returns zao za mwaka wanapewa upendeleo maalum wa kutiliwa mapesa kwenye returns zao kwa vile mafuta yanachimbwa hapo. au angalia vipi watu walishughulikiwa katika kadhia ya kuvuja kwa mafuta huko Louisiana. rais Obama alikemewa kama mtoto mdogo, na bp wakashughulikia suala hilo kwa adabu kabisa. sisi waafrika bado tunataka kuendelea kuendeshana kinguvu nguvu tu, hatuoni kwamba tunawaponza hata polisi wetu wawe ni wapigaji tu na ndio na wao sasa wanapigwa. bado watanzania tunadhani rais au mawaziri wake ndio watu pekee wenye busara na katika maamuzi yao hawafanyi makosa. jamani the world now has become so small because of technology, watu wako so faster kujifunza kwa watu wengine, mambo mengine hayahitaji hata degree za chuo kikuu just no brainer. serikali inapaswa kueleza comprehensive scheme zake za kimaendeleo ili wananchi wazielewe, wananchi wameichagua serikali kuwaongoza na si kuwatawala. angalia wenzetu wa US wanaita Reagan au Obama administration na sio rule wala regime. amani tuliyonayo sidhani kama kwa 100% ilipatikana kwa busara za viongozi pekee, bali kwa 80% naamini imepatikana kwa ustaarabu wa asili wa watu wa Tanzania. watu wanapotoa madai yao tusiwachukulie tu kwamba hawana akili, wachochezi, wahuni na wahujumu nchi bali tuzingatie na kutafuta ufumbuzi wa kufaa- meaningful and appropriate solutions hata kama haitomfurahisha kiongozi. kwa mwelekeo ninaouna sasa nchi inaelekea kubaya, na Mwenye Enzi Mungu atunusuru lakini pakitokea machafuko yatakayoiharibu nchi ni viongozi ndio wa kulaumiwa. viongozi wasio na busara always put their countries into risks. nadhani viongozi wa kiafrika wamuombe mzee Mandela awape semina/darasa la namna ya kuongoza katika karne ya 21 kabla hajaondoka duniani (MUNGU AMPE UMRI MREFU)kama tulikuwa tunasoma tu kwenye vyombo vya habari vurugu za Rwanda, Somali, sudani, nk basi Tanzania haiku mbali na hali hio na labda vurugu za Mtwara zitakuwa ni wakeup call na kipimo how wise these leaders are in taking care of business.

Anonymous said...

Thanks previous poster, with due respect ningependa kukujulisha kuwa, kama wewe ungelikuwa unafuatilia siasa za Wamarekani usingeweza kutoa mfano wa jinsi rais wa Marekani anavyoitwa na wamarekani maana ungejua kuwa kuna watu wengi wanamwita Rais wa Marekani mwuaji kama Hitler, Msoshalisti myangang'nya mali kutoka kwa matajiri kuwapa maskini. Kumbuka kuwa wanaofanya wananchi wamwite hivyo ni hao matajiri ambao mfumo wa kibepari umewafaa lakini wanataka kufaidika zaidi kwa kuwa ubepari bila sharia ni kimbari ya kiuchumi. Pale hao wanaoona maslahi yao yametetereka ndipo huanza kutumia hata zile fedha walizozipata kwa faida ya mfumo kutaka kupata zaidi badala ya kuzihifadhi ziweze kuendeleza biashara zao kihalali. Kwa nchi yetu Tanzania ni kwa kupitia wanasiasa na kwa kioo cha wanaoita majina viongozi, wanasiasa ambao kwa Tanzania ndio wafanya biashara, msongo ni huo huo. Na pia pale kiongozi wa nchi ambazo si za magharibi anapokaa madarakani kupita muda ambao nchi za magharibi zinakadiria kuwa ni wa kutosha kiongozi kukaa madarakani, basi huyo ataitwa mtawala wa nchi ingawa kwa mtazamo wangu hayo ni maneno au majina tu na sisi tunaoyatafsiri ndio tunaguswa na ukweli. Kwa Demokrasia iliyokomaa, hata Raisi wa America anaitwa majina dhalilifu lakini kwa kuwa ni ukomavu kidemokrasia hakuna anayejali. Ni halali kumwita kiongozi yeyote aliyekatika utawala Fulani na ni halali kuuita utawala wowote regime kwa kuwa maana halisi ya maneno hayo ni ya zamani na yule anayetafsiri ndiye mwenye burden ya kuweka hisia zake. Marekani wakiamua kumuita Raisi yeyote Ruler wanahaki hiyo na hasa inapokumbukwa kuwa hata katika mahakama zetu huwa tunakwenda kupata kutafsiriwa rules zetu wenyewe pale ambapo pande zozote husika zinapodai kuwa kwa utofauti wao kila mmoja ana haki iliyokiukwa na mwingine.Nikirudi kwa kinachoendelea Mtwara na Tanzania kwa ujumla, na kwa busara kidogo, mgogoro wa Mtwara ni lazima uangaliwe kwa mtazamo japo mdogo kwa kuanzia, Tanzania kama familia tujiulize, hata kiongozi yeyote wa familia kufuatana na kipato hawezi kuwafanyia mambo makubwa watoto wake wote kwa mara moja. Kwa serikali ni kwamba tuna advantage kuwa kwa kutumia bunge, wabunge wanaweza kuishinikiza serikali kuleta au kuharakisha maendeleo si kama katika familia pale mototo anayehisi hajatendewa haki hawezi kwenda kokote na akitaka kudai haki yake basi akiwa na bahati atatakiwa kuondoka nyumbani akaishi peke yake. Na ikumbukwe kuwa katika vitu atakavyokuwa na uchaguzi navyo hakuna kunachosema fanya fujo,choma moto gari la baba yako moto. Kwa watu wa Mtwara, ikumbukwe kuwa kuna utawala wa sharia na utawala wa sharia unaishia kwenye utekelezaji ambao nguvu hutumika. Kuna viongozi wameshindwa kuwawakilisha na sasa wanawashauri mfanye fujo ili kutia mvuto wa kisiasa badala ya kuwa shauri nyinyi mfuate sharia katika kudai maendeleo yenu mnayostahili kihalali.Bila kubomoa miundo mbinu ambayo serikali imegharimia kuijenga.Hata hilo bomba litajengwa kuanzia Mtwara kwa nini msisubiri lijengwe basi wakati mnaendelea na mchakato wa kudai haki zenu za maendeleo bungeni? Hata hapa Marekani ukiandamana na kuhatarisha maisha ya raia yeyote awe anahusika na maandamano yako au la, utakumbana na mkono wa sharia basi ni vizuri tuact baada ya kufanya utafiti kwa maana hakuna serikali ambayo itaacha hali iendelee kuchafuka eti kwa kuogopa mashinikizo. Hapa Marekani wanaoandaa matayarisho ya maandamano huwa wanafedha za kuwawekea dhamana washiriki,kuwalipa kiasi cha fedha mara wanapoathirika na matokeo ya maandamano yao lakini mara nyingi waandamanaji hawana uwezo kisheria kuishitaki serikali kuu moja kwa moja. Kwa watu wa Mtwara, nani anawalipa wakifanya vurugu? Ni lazima Watanzania tuwe makini kuona kilicho ndani bila kughadhibika kutoa lawama. Ahsanteni Sana.