ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 27, 2013

WARSHA YA UTENGENEZAJI FILAMU- MAOMBI YAFUNGULIWA

ZIFF sasa inapokea maombi kutoka kwa watengenezaji filamu Afrika Mashariki wanaotaka kushiriki katika warsha ya utengenezaji filamu wakati wa ZIFF mwaka huu..
Wanafunzi 5 (mmoja toka kila nchi ya Afrika Mashariki) watalipiwa safari, malazi na chakula ili kushiriki kwenye warsha hiyo. Wanafunzi 5 wengine watajilipia wenyewe.
Mfumo wa warsha utakuwa ni kufuatilia kikundi cha watengeneza filamu walio tayari mafundi watakaokuwa wanatengeneza filamu fupi wakati wa ZIFF. Utengenezaji huu unaitwa Guerilla Filmmaking (yaani filamu chapchap) na katika siku 6 filamu itapigwa, itahaririwa na kuonyeshwa ZIFF siku ya mwisho.
Wanaotaka kushiriki kwenye warsha watume maombi yao hivi:
CV fupi.
Maelezo kwa nini wachaguliwe (maneno 1000)
Maombi yatumwe kwa: workshop@ziff.or.tz
Warsha imedhaminiwa na Goethe Institute na GIZ (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani) na Jumuia ya Africa Mashariki (EAC)
Maelezo pia yako www.ziff.or.tz 

No comments: