ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 31, 2013

MARQUEE CLUB KUINGIA NI MIAKA 21 KWENDA JUU, LAKINI JUSTIN BIEBER ALITINGA NDANI PESA HUVUNJA SHERIA POPOTE PALE

Justin Bieber akiingia Club Marquee NY usiku huo, Club nyingi New york ni kuanzia miaka 21 na ukiwa chini ya hapo ni nyumbani chini ya shuka kulala. Ingawa zipo zile unazoruhusiwa kuanzaia miaka 19 na ni siku moja kwa wiki ambayo ni alhamisi pekee kama Webster Hall Club na pia uwezi kuuziwa kilevi. Lakini uwezi kwenda hapo kama unataka kufurahia usiku wako na hasa kama umevunja kabati kwa nguo ya kutokea usiku huo ni lazima uchagua club ambayo ukiingia unasema uko club ndani ya Jiji la wasilo lala New York City unaingia Club saa 6 usiku na unatoa saa 1 asubuhi. Moja ya Club zinazo bamba ndani ya New York ni kama hii.
Justin Bieber alikuwa New York kwa ajili ya Earth premiere Movie hapa kiingia Club Marquee
Hapa ndiyo  Club Marquee mambo huwa hivi Justin Bieber akutaka kukosa mambo haya ingawa umri unambana kuwa hapa, na inasemekana kabla ya kuingia hapa alianzia Avenue Nightclub nayo ni club maarufu sana ukiachia hile ya Jay'z 40/40 club New York City.
Hawa ni kati ya warembo ambao Bieber alikuwanao usiku huo katika club hiyo ya marquee
Marquee Club bila kujiandikisha kwenye guestlist kuingia hapa ni mbinde piga simu mapema hili kupata nafsi ya kuingia bila hivyo utaambiwa nunua meza kwanza ndiyo upate kipawa cha mbele kuingia.


No comments: