Sunday, May 26, 2013

MISA KWA LUGHA YA KISWAHILI , DMV

Ndugu Watanzania na Wote wapenzi wa Lugha ya Kiswahili. Ni tumaini kubwa kuwa Tumesherehekea vizuri Pentekoste, Utatu mtakatifu na tunajiandaa vyema kusherehekea Mwili na Damu Takatifu ya Yesu Jumapili ijayo.
 
Kwa mara nyingine tunawakaribisha kushiriki Misa Takatifu kwa Kiswahili lugha ya Taifa letu na ya Kimataifa pia.
 
Lini?        June 16, 2013 saa 8:30 Mchana
Wapi?      St. Camillus Parish
                1600 St. Camillus Drive
                Silver Spring, MD 20903
Nani?       Mtanzania yeyote. Yeyote anayezungumza kiswahili. 
Nia:-  Kujiombea sisi tulioko ughaibuni na Familia zetu, Kuliombea taifa letu amani na Kumshukuru Mungu kwa Baraka tulizojaliwa. 
Pia tutachagua Viongozi wa Jumuiya yetu. Tafadhali kama uko Tayari kutusaidia katika uongozi nipe jina lako mapema.
Naomba tutoe taarifa hii kwa wenzetu wote. 

Asanteni Sana 
 
Wenu Padri Evod Shao na Kamati ya Maandalizi

No comments: