Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Charles Kitwanga
Dodoma. Serikali ipo katika mpango wa utekelezaji wa mradiwa usambazaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano awamu ya tano.Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Charles Kitwanga ambaye alisema mradi huo unalenga kuziunganisha wizara, idara, vyuo, shule, hospitali na taasisi za umma kwenye mkongo.
Alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni taasisi hizo kushindwa kujiunganisha kutokana na uwezo mdogo wa kifedha,ambapo alisema tangu Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ulipoanza kutumika umesaidi kushusha gharama za mawasiliano kwa watumiaji.
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Magreth Mkanga (CCM) aliyetaka kujua lini mkongo utaanza kutumika, kama utasaidia kupunguza gharama za mawasiliano na pia Serikali imejiandaa vipi kuwawezesha wananchi kunufaika na mkongo huo hata wale wasio na uwezo.
Naibu Waziri alitoa mfano kushuka kwa gharama za kusafirisha masafa kwa asililimia 99 kutoka Dola za Marekani 20,000 kwa mwezi kwa umbali wa kilometa 1,000 kwa mwendo kasi wa Megabits mwaka 2009 hadi kufikia Dola za Marekani 160 kwa mwezi kuanzia mwaka 2011.
“Huduma za intaneti zimeshuka kutoka Sh36,000 kwa Gigabyte moja mwaka 2009 hadi Sh9,000 kwa Gigabyte moja mwaka 2013 sawa na kushuka kwa asilimia 75,” alisema
Mwananchi
No comments:
Post a Comment