ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 1, 2013

MSIBA DMV NA TANZANIA

 
Mzee Alfred Tandau Enzi ya uhai wake
Watoto wa marehem,  Uwezo Tandau na Andrew (K.P)Tandau waishio DMV wanasikitika kutangaza kifo cha baba yao, mzee Alfred Tandau kilichotokea Tanzania April 30, 2013. kama ilivyo ada, mila na desturi yetu kupeana pole ni wajibu na ukarimu wetu. upatapo nafasi fika nyumbani kwa wafiwa hapa Maryland kwa address hii:
17 Gas Light Court, 
Gaitherburg, Md 20879.
Kwa maelezo zaidi pia unaweza kupiga simu kupitia number hizi,
Andrew Tandau 
# 240 421 8392. 
Uwezo Tandau
 #240 476 0094. 
Jacqueline Korassa
 # 240 706 6831.

Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mweka Hazina wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Marehemu Alfred Tandau


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kushtushwa na kusikitishwa kwake na taarifa za kifo cha aliyekuwa Mweka Hazina wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kiongozi wa miaka mingi wa wafanyakazi na Waziri wa muda mrefu wa Serikali, Mheshimiwa Alfred Tandau ambaye ameaga dunia jioni ya leo, Jumanne, Aprili 30, 2013.
Katika salamu zake kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Abdulrahaman Kinana, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amesema:
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mzee Alfred Tandau ambaye nimejulishwa kuwa amepoteza maisha jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu ya kansa ya tumbo.”
“Nilimfahamu Mzee Alfred Tandau kwa miaka mingi. Alikuwa kiongozi hodari na mwaminifu ambaye katika nafasi zote alizozishikilia katika utumishi wake wa umma alithibitisha uadilifu na uzalendo wa kiwango cha juu,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:


“Katika uongozi wa Chama cha Wafanyakazi cha NUTA na baadaye JUWATA, Mzee Tandau alijipembenua kama mtetezi halisi na mkweli wa maslahi ya wafanyakazi. Katika Serikali ambako alitumia kwa miaka mingi kama Waziri alikuwa mwaminifu na mtii kwa Serikali yake, kwa viongozi wake na kwa wananchi aliowatumikia. Katika nafasi yake ya Mweka Hazina wa CCM aliendeleza sifa hizo hizo alizokuwa nazo tokea nyuma. Tutakosa sana busara na ushauri wake.”


Ameelezea Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Kinana salamu zangu za dhati za rambirambi kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako nawatumia rambirambi viongozi na wanachama wote wa CCM kwa kumpoteza kiongozi na mwanachama mwenzao.”


Amesisitiza: “Aidha, kupitia kwako, naomba unifikishie salamu nyingi za pole kwa familia kwa kuondokewa na kiongozi na mhimili wake. Wajulishe kuwa niko nao katika kuomboleza kifo cha kaka yetu na kiongozi mwenzetu na naelewa machungu yao katika kipindi hiki. Napenda wajue kuwa naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya marehemu. Amina.” 


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM

No comments: