ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 15, 2013

Msondo,Che Mundugwao,Majuto kuwasha moto Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania Mkwakwani Tanga tarehe 19.05.2013


Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 wakiwa katika Picha ya Pamoja

Baada ya shamlashamla na mapokezi makubwa ya Miss Utalii Tanzania walipo ingia Mkoani Tanga na kupokelewa na umati mkubwa wa watu, warembo hao wapo kambini tayari kwa maandalizi ya Fainali hizo.
Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania zitafanyika Tarehe 19.05.2013 Mkoani Tanga ambapo warembo zaidi ya 30 watapanda Jukwaani kuwania Taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013 ndani ya Mkwakwani.
Sambamba na Fainali hizo za Miss Utalii , kutakuwa na Burudani ya Kukata na shoka ambayo itasindikizwa na Bendi kongwe ya Muziki Msondo Ngoma kutoka Dar es salaam, Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao, Majuto Arts Group, Mdumange, vikundi vya ngoma na Sarakasi.
Fainali za Taifa zitaanza kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 jioni Ambapo viingilio kwa watoto itakuwa 2,000 na wakubwa 5,000 Baada ya hapo kuanzia saa 1 usiku hadi Majogoo viti Maalum itakuwa ni 20,000 na kawaida itakuwa 10,000
Mpaka sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini ,wanajiandaa vizuri kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia na nchi yatakako fanyika katika mabano International Miss Tourism World (Marekani), Miss Tourism United Nation (Mexico), Miss Heritage World (Tunasubiri Taarifa), Miss Tourism University World(Tanzania), Miss Globe International (Uturuki), Miss Tourism World ( Equatorial Guinea ), Miss Freedom Of The World ( Kosovo) , na Miss Tourism United Nation (Nigeria) n.k
Wakati huohuo, katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya Fainali za taifa, za mashindano hayo ambapo mkoa wa Tanga unakuwa wenyeji kwa mara ya kwanza yanafanyika kwa ubora na hayakwami, kamati ya maandalizi ya kimkoa umeundwa ambayo mwenyekiti wake ni Peter Semfuko Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga. Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism

Model Of The World 2008-Personality, Miss Africa 2006 – 1ST Runner Up n.k

No comments: