Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa hiari wa PSPF Bi. Zuhura Lwamo akipokea fomu ya usajili ya Mpango huo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA ndugu Irene Isaka baada ya Mkurugenzi huyo kujisajili katika Mfuko huo.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa PSPF Ndugu Queen Edward akielezea wajumbe wa Bodi ya udhamini ya SSRA shughuli na fursa mbalimbali zilizopo katika Mfuko wa PSPF
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni PSPF Ndugu Gabriel Silayo akielimisha wabunge juu ya shughuli mbalimbali za Mfuko wa PSPF katika Semina iliyofanyika tarehe 12/05/2013 bungeni, Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mh. Adam Malima akipata maelezo kuhusu mpango wa wa uchangiaji wa hiari wa PSPF na maafisa wa Mfuko huo.
Kaimu Meneja wa Idara ya Mafao PSPF ndugu Hajji Moshi akielimisha wadau wa Mfuko kuhusu mikopo ya nyumba itolewayo na Mfuko huo
Afisa Uwekezaji wa PSPF ndugu Hamidu Ngororo akiwaelezea wajumbe wa Bodi ya udhamini wa SSRA kuhusu nyumba zilizojengwa na Mfuko huo kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wake.
Meneja Mawasiliano na Masoko ndugu Costantina Martini akielezea juu ya Mfuko wa PSPF na fursa zitolewazo na Mfuko huo kwenye semina ya waandishi wa habari Dodoma Hoteli
Mbunge wa jimbo la Chamwino Mh. Chibulunje, akipata taarifa muhimu za usajili kuhusu mwanachama wa PSPF ambaye anaishi katika jimbo lake.
Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment