ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 15, 2013

Skylight Band yazidi kukusanya maelfu ya mashabiki ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.

Binti mwenye kipaji cha aina yake Mary Lukas akiongoza waimbaji wenzake kutoa burudani Ijumaa iliyopita kwa mashabiki wa Skylight Band katika kiwanja chao cha nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar.
Wapenzi wa Skylight Band na staili ya aina yake baada ya kuamua kutinga ukumbi na Vest hii ikimaanisha hawataki kusikia joto wakati wa kusakata muziki wa Band hiyo inayobamba nchini Tanzania.
Uzao wa BSS Mary Lukas akifanya yake jukwaani, Ewe Mtanzania Mary Lukas anaomba kura yako amechaguliwa kushiriki tuzo za Kilimanjaro Music Awards katika Category ya Mwimbaji Bora wa kike wa Band...Mpigie kura andika AM4 tuma kwenda namba 15345.
Watu wa ukweli wenye mapenzi ya kweli na Skylight Band...Wewe Je? Njoo Ijumaa hii ujionee vipaji.
Sam Mapenzi wa Skylight Band akivuta hisia kali wakati akitoa burudani kwa wapenzi wa Band hiyo.
Vijana wa Skylight Band wakimwimbia nyimbo ya Happy Birthday mmoja wa shabiki wa band hiyo aliyefahamika kwa jina la PAPITO, Ijumaa iliyopita ilikuwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Shabiki wa Skylight Band PAPITO akikata cake yake mbele ya jukwaa tayari kuwalisha wanamuziki wa band hiyo.
Birthday Boy PAPITO akimlisha cake mmoja wa marafiki zake.
PAPITO akimlisha cake Sam Mapenzi wa Skylight Band aliyewakilisha kikosi kizima cha Band hiyo. Mdau na wewe unakaribishwa kusheherekea Birthday yako pamoja na Skylight Band Ijumaa hii.
Rappa Joniko Flower akitoa burudani kwa wapenzi wa Skylight Band... Joniko ni miongoni mwa waimbaji bora wa kiume wa band aliyechaguliwa kushiriki tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2013 anaomba kura yako wewe Mtanzania andika BG4 au AX3 tuma kwenda namba 15345.
Mwanamuziki mkongwe aliyewahi kuwa Jaji wa shindano la Bongo Star Search Mzee John Kitime akichukua matukio ya kumbukumbu huku akionyesha furaha ya aina yake kuona vipaji vya wanamuziki wa Skylight Band husuani Mary Lukas mshiriki wa BSS.
Mashabiki waliotia fora Ijumaa iliyopita baada kuja ukumbini hapo na Vest maalum kwa kusakata Sebene la Skylight Band ili wasisikie joto.
Aneth Kushaba AK 47 akitoa burudani kwa wapenzi wa Skylight Band huku akisindikizwa na Sony Masamba pamoja na Mary Lukas.
Aneth naye ni miongoni Waimbaji bora wa kike wa Band wanaowania Tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2013 naye yeye pia anaomba kura wewe Mtanzani mpigie sasa kwa kuandika AM 1 tuma kwenda namba 15345.
Muziki wa Carolina unapokelea inakuwa hivi kwa fans wa Skylight Band.
Sam Mapenzi akionyesha ufundi kwa mashabiki wa band hiyo huku nao wakimuiga miondoko yake.
Kikosi kazi cha Skylight Band kikitawala Jukwaa na manjonjo ya aina yake.
Mashabiki walipagawaje na Sebene la Skylight Band.
Hapana chezea Skylight Band wewe....ni balaaa. Vibonge wepesi wakijimwaga na sebene.
Uliwadia ule muda wa Skylight Band kutambulisha nyimbo yao mpya ya mduara inayotambulika kama"Umechana Mbeleko".
Mashabiki wakizungusha nyonga wakati wa kucheza mduara.
Hapo sasa wa mbele aende mbele wa nyuma arudi nyuma....
Mashabiki wakionekana kuchizika na wimbo huo mpya wa mduara wa band hiyo na kupiga makelele urudiwe tena na tena....Njoo Ijumaa hii uonje ladha yake.
Mrembo wa ukweli katika pozi matata mbele ya camera yetu.
Kadri siku zinavyokwenda Skylight Band inazidi kuongeza namba ya mashabiki wa band hiyo kwa kasi ya ajabu, baadhi yao ni hawa hapa.
Fans wapya wa Skylight Band wakishow love.
Picha juu na chini ni William Malecela wa Blog ya Jamii a.k.a LE MUTUZ akishow some love na Mabebsss wa ukweli.

No comments: