Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi.
Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akisalimiana na Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa mara baada ya kuwasili kuzindua tawi jipya la ofisi za DStv Tanzania lilolopo Kariakoo barabara ya Msimbazi karibu na Diamond Trust Bank jijini Dar. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Multichoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi mara baada ya kuwasili. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Multichoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akiwakaribisha wageni waalikwa na wakazi wa jijini Dar kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa tawi jipya la Ofisi za DStv zilizopo Karikakoo barabara ya Msimbazi karibu kabisa na Diamond Trust Bank ambapo amesema Mutlichoice Tanzania inawajali wateja wake ndio maana imeamua kusogeza huduma hizo karibu na wateja wake na kuwataka Watanzania kujipatia king'amuzi cha DStv pamoja na huduma ya ufungaji kwa bei poa ya Tshs 149,000 tu ofa hii ni kwa kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 13th May mpaka 18th May, 2013.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Multichoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua tawi hilo katika sherehe zilizofanyika jana jijini Dar.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Ofisi za DStv zilizopo Kariakoo barabara ya Msimbazi karibu na Diamond Trust Bank jijini Dar.
Mstahiki Meya Jerry Silaa amewapongeza Multichoice Tanzania kwa kuwa wakongwe wa Digitali Tanzania na kuwataka kuendelea kutoa huduma bora zenye viwango ili kuendelea kuwa vinara wa kutoa huduma ya Digitali Tanzania na pamoja na hayo amefurahishwa kusogezwa karibu kwa huduma DStv katikati kabisa ya jiji zitakazowasaidia wakazi Manispaa ya Ilala.
Picha juu na chini Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wakimsikiliza mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la Ofisi za DStv Tanzania zilizopo barabara ya Msimbazi Kariakoo karibu na Diamond Trust Bank. Kulia ni Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Multichoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kufungua rasmi tawi jipya la Ofisi za DStv Tanzania liliopo barabara ya Msimbazi Kariakoo karibu kabisa na Diamond Trust Bank. Anayeshuhudia tukio hilo ni Branch Coordinator Prosper Sangawe.
Mgeni rasmi stahiki Meya Jerry Silaa akifanya malipo ya akaunti yake ya King'amuzi cha DStv kwa Ezekiel Mwasuluko wa kitengo cha Huduma kwa wateja katika tawi hilo jipya kuashiria ufunguzi rasmi na utoaji huduma umeanza kazi.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha ankara yake ya malipo kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani).
Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakipiga makofi baada ya tukio hilo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mutlichoice Tanzania baada ya kuzindua rasmi tawi jipya la kutoa huduma kwa wateja wa DStv lililopo barabara ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar.
Kijana mtanashati Ezekiel Mwasuluko Multichoice Tanzanua wa kitengo cha huduma kwa wateja akiwa tayari kukuhudumia wewe Mtanzania katika tawi lao jipya la Ofisi za DStv barabara Msimbazi Kariakoo jijini Dar.
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo (mwenye miwani nyeusi) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake nje ya Ofisi mpya za DStv zilizopo maeneo ya Kariakoo barabara ya Msimbazi karibu na Diamond Trust Bank.
Meneja Masoko ya Multichoice Tanzania Furaha Samalu na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi na Revina Bandihai katika pozi matata kuonyesha furaha ya ufunguzi wa Tawi lao jipya lililopo Kariakoo barabara ya Msimbazi karibu na Diamond Trust Bank.
Muonekano wa nje wa Ofisi za DStv Tanzania zilizopo barabara ya Msimbazi - Kariakoo karibu kabisa na Diamond Trust Bank jijini Dar es Salaam.
Vibajaji vya DStv vikiwa tayari kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji kutoa huduma kwa wateja wao.
No comments:
Post a Comment