Prof. Rwekaza Mukandala
WAKATI Serikali ikitangaza kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.
Habari za kuaminika zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.
Naye Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Philipo Mulugo alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo iliita bila ya kupokelewa na baadaye akatuma ujumbe mfupi akisema, "Sorry I'm busy call back later", alisema Mulugo kupitia simu yake ya mkononi.
11 comments:
Kudadadadadadadadadadadadadeki! Yani kama ni mpira wa miguu, tungesema refa kiziwi, mshika kibendera kipofu.
safi sana prof.mukandara na dk joyce mm nawauunga mkono maamuzi yenu asilimia mia moja serikali hii ya ajabu sana wao ndio walipitisha matokeo hayo tena waziri wa elimu ndio aliyatangaza mbele ya waandishi wa habari kama waliiona yana mapungufu kwa nn wasiyasimamishe mapema,wanakuja kutuletea siasa mbele ya elimu hapa.
Hii ndio Tanzania, usishangae.
Unajidhalilisha mtuma comment, unaonesha unaitikadi ya mlengo wa cha chenye vurugu, chama cha kaskazini, chama cha wasiokuwa na hoja bali lawama wakati wote, chama cha kufitinisha wananchi na serikali yao kwa kutumia shida zao, mfano mtu akikosa chunvi, sabuni, dagaa, mchicha, dekio la nyumbani kwake, dawa hospitali, mhalifu mmoja kusafirisha wanyama pori nje ya nchi n.k yote mchawi ni Serikali !, jamani mnatakiwa kujiuuliza hapo mlipo mnaifanyia nini Tanzania badala ya kulaumu uchwara, achani hizo.
Tunahitaji wakina Mukandalla kama Kumi hivi ili tuweze kuendelea. Maana haiwezekani Leo upitishe majibu alafu kesho ubadilishe. Msimamo lazima uwe mmoja katika makubaliano especially kwenye vitu kama hivi. Inamaanisha serikali haikuwasiliana na Necta kwenye uamuzi huu. Kweli watu wapo busy na siasa na wanasahau ukweli.
Mmh hicho chama chenye hoja toka miaka 50 ya uhuru mbona hatuoni matokeo ya mafanikio kama nchi? Sidhani kama wewe anon unatofuti na hao unaolalamika ni wafujo. Afterall umeshaweka lebo ya ukanda, jamani hamchoki na siasa za ubaguzi? Hamuoni matokeo ya siasa za udini. Nivizuri kukubali critism nakuzifanyia kazi.
Unanishangaza mtuma comment, hapa hatujadili maswala ya chama wala kutupiana lawama.kama ni matokeo yalishatoka na ninaimani vigezo vyote vilifatwa katika kutoa matokeo hayo.kitendo cha serikali kutaka kurekebisha matokeo hayo ni dhairi kua wanajikosoa na hawana imani na watendaji wao.
achana na masuala ya vyama hapa chama na matokeo ya kidato cha nne wapi na wapi.tuzungumzie suala hili kwa maslahi ya taifa letu. sasa tukisema sasa hivi tufute matokeo sasa wale waliofeli miaka mingine na wenyewe wakidai matokeo yao pia yafutwe atalaumiwa nani?
watu hawawi waelewa kwa nini kama serikali ndio ilipitisha na ndio imeamrisha mchakato urudiwe kwa nini mnataka kupingana na kauli ya mwisho kumbukeni mwaka jana matokeo yaliyokosewa watu walitakiwa wajiuzulu lakini wakang'ang'ania kama wanapingana na serikali wajiuzulu tuuuuu kwa nini wang'ang'anie unataka kupingana na serikali jamani
HONGERA, HONGERA,HONGERA, HONGERA! PROFESSOR,
Huo ndio ujasiri na ndio Usomi.
1. Haiwezekani kupeleka Mizigo Advance na Vyuo vya Ualimu na baadaye serikali ije kutulaumu Walimu kuwa Hatufundishi na huku kujisahau kuwa walipeleka WALIOCHAKACHULIWA!!! KERO!!!!!
2. Serikali imesahau na haina kumbukumbu kuwa hao ndio waliopewa msamaha wa serikali wa kupita kidato cha pili bila kurudia????
3. Hebu tufike wakati tusilete siasa kwenye Elimu. Ni sawa na mtu kujijaribishia kuji-shoot na silaha eti una-serve life.
HONGERA PROFESSOR M na JOYCE NDALICHAKO kwa kutumia akili yenu ya Kisomi mliyoipata.
TUKO NYUMA YENU TUNAUNGANA NANYI MSIOGOPE VITISHO.
Malipo mbinguni ni sawa.
Wasituletee Mizigo Advance na Vyuoni tuhagaike nayo wakati
maisha walimu tunataabika nayo.
Mwalimu S
Hongereni sana NECTA huo msimamo wenu mzur.Kama serikal inataka wasomi halali basi isiangalie wingi wa watu waliofaulu bali viwango vya watu waliofaulu.
Post a Comment