Thursday, May 2, 2013

PITA PITA YA VIJIMAMBO NEW YORK CITY 125 ST UP TOWN HARLEM

Hapa ni Apollo, Apollo ni sehemu maarufu sana New York City umaarufu unakuja kwasababu masuperstar wengi sana wamarekani wamepitia hapa iwe wale wachekeshaji au wanamuziki. Sehemu ni kituo cha kuonesha kipaji chako na ukikubarika hapa ndiyo safari ya kuwa maarufu inanukia. Apollo panakuwa na show kama hizo kila siku ya jumatano kuanzia saa tatu usiku hadi saa sita.
Watu wakiwa tayari kwenye line kutaka kuingia humo ndani kushuhudua moja ya maonyesho ya siku hiyo ya jumatano.
Siku ya jumatano hujulikana kwa jina hilo la AMATEUR NIGHT kama unavyoona katika kibao kilichopo mbele ya jengo hilo la Apollo New York City.

No comments: