ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 17, 2013

Reli mpya kujengwa Dar es Salaam

Pia wizara inaangalia uwezekano wa kuanzisha huduma maalumu ya kati ya Stesheni ya Dar es Salaam na Gongo la Mboto kwa ajili ya kuhudumia abiria wanaoshukia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Dk Mwakyembe alisema hivi sasa wanatafuta mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma ya usafiri wa treni ya abiria katika jiji la Dar es Salaam.
“Mwekezaji huyo atatumia miundombinu ya reli iliyopo, vichwa vya treni na mabehewa maalumu kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Jiji,” alisema Dk Mwakyembe, ambaye Wizara yake imeomba Sh491,105,994,000 katika bajeti hiyo, Sh100,584,174 zikiwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh390,521,220,00 kwa shughuli za maendeleo.
Alisema usafiri wa reli Dar es Salaam umesaidia kupunguza idadi ya magari barabarani kwani abiria 14,000 wanaotumia reli hiyo kwa siku wangehitaji mabasi 467.
Alisema wizara yake imetenga Sh113.1 bilioni kwa ajili ya kukamilisha ununuzi wa vichwa vinane vya treni, mabehewa 22 ya abiria, mabehewa 274 ya mizigo na mabehewa 34 ya breki.
 Magari ya Noah
Dk Mwakyembe pia alizungumzia suala la matumizi ya magari ya aina ya Noah kubeba abiria na kuitaka Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini,(Sumatra) kuandaa utaratibu wa kutoa leseni kwa magari hayo. Alisema ingawa Sumatra waliyazuia yasibebe abiria kwa kuwa hayakuundwa kwa ajili hiyo, alitaka wabunge wakumbuke kuwa adha ya usafiri nchini ambayo imeilazimu Serikali kuruhusu pikipiki za magurudumu matatu na mawili kubeba abiria.
“Kabla ya kutoa leseni ni lazima Sumatra iandae masharti ya kurekebisha madirisha ya gari ya Noah hasa yale ya upande wa nyuma na kupanga nauli elekezi,” alisema.
Mwananchi

No comments: