Mwandishi na Mpigapicha Mkuu wa Global Publishers, Richard Bukos, akisalimiana na Zombe baada ya rufaa hiyo kutupiliwa mbali.
Bukos akiwa na ‘kampani’ ya Zombe, mahakamani hapo, wa pili kushoto ni mke wa Zombe na wa pili kulia ni shemeji yake Kamishna huyo mstaafu.
MAHAKAMA ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, ACP, Abdallah Zombe. Akitupilia mbali rufaa hiyo, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Elizabeth Mkwizu, alisema kuwa Notice ya kupeleka rufaa hiyo ilikuwa na mapungufu ya kisheria. Licha ya kuitupilia rufaa hiyo, Mkwizu aliwaambia mawakili wa serikali kuwa bado wanayo haki ya kuomba tena rufaa ya kesi hiyo kupitia sheria ya ukomo wa muda.
(PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
1 comment:
bongo siku hizi wadada wote waarabu?
Post a Comment