Advertisements

Wednesday, May 22, 2013

Siku Yanga alipomaliza ligi kwa ushindi dhidi ya mpinzani wake wa jadi Simba

Yanga waliishinda Simba sc baada ya kuibamiza bao 2-0 kwenye pambano la kufunga msimu wa ligi kuu Tanzaia bara lililopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ushindi huo umeifanya Yanga kusherekea taji la 24 la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara bila shaka yoyote.
Hakika kipigo hicho kiliwaduwaza mashabiki wa simba sc walio hudhuria pambano hilo uwanja wa Taifa na kuondoka kichwa chini bila kuamini kilicho tokea mbele yao.
Pia wanariadha mbali mbali nchini Tanzania walichuana kikamilifu kwenye mbio za wazi zilizo fanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mbio hizo ziliweza kuwashirikisha hata watoto wadogo wenye miaka 12 hadi 14 ambao walichuwana kwenye mashindano hayo.

No comments: