ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 24, 2013

Taarifa ya Jeshi la Polisi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                    Ofisi  Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                   Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                  S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                               DAR ES SALAAM.
 
24 MAY 2013
 
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi Nchini linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa uchochezi na chuki kwa wananchi na viongozi wa serikali kwa njia ya simu ya mkononi akituma SMS kwa lengo la kuchochea fujo, vurugu na kutoa matusi kwa viongozi hao.

Mtu huyo amekuwa akifanikisha kazi hiyo kwa kutumia Chips (sim card) 13 za simu za mkononi ambazo amekamatwa nazo. Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtu huyo na ushahidi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zingine za wahalifu kama hao kujitokeza na kutoa taarifa hizo polisi ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki, wakiwemo watu wanaowashawishi wenzao kwa njia ya fedha, kuwashauri ama kuwasaidia kwa namna yeyote ile katika kufanikisha uhalifu huo na kusababisha uvunjifu wa amani hapa nchini.
Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria za nchi.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

1 comment:

Anonymous said...

majungu matupu.