Sunday, May 19, 2013

Tano Bora ya wabunge wazalendo kwa taifa letu!

Habarini wana jf, kwa hali ya mambo inayoendelea katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni wazi kuwa wabunge wengi wamepoteza sifa ya uwakilishi kwa wananchi katika jengo lile la bunge mjini dodoma, wabunge wengi wameonekana kuwa wasemaji wa serikali na si wa wananchi! Kufuatia hali hiyo kwa uchunguzi wangu usio rasmi, nimegundua wako baadhi ya wabunge wachache bado wana moyo wa uzalendo kwa wananchi na taifa lao kiujumla! Wafuatao ni wabunge watano bora kwa uzalendo na utumishi uliotukuka kwa wananchi wao waliowatuma bungeni:

1. Mh. Tundu Lissu(chadema)-singida mashariki.
2. Mh. John Mnyika(chadema)- Ubungo.
3. Mh. Deo Filikunjombe(ccm)-Ludewa
4. Mh. Kangi Lugora(ccm)-Mwibara.
5. Mh. Halima mdee(chadema)-kawe!

Pongezi ziende kwa wananchi waliotuchagulia wabunge hao, pia pongeze ziende kwa waheshimiwa wahusika! Mungu awalinde na kuwapa baraka zake! Nawasilisha.

1 comment:

Anonymous said...

umemsahau msigwa wa iringa ni kiboko yule jamaa