Bw.Suleiman Saleh Afisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC akiwa katika picha ya pamoja na Bibi Lilibeth Defiesta Asera ,Meneja Miradi wa Mji wa Valejo,California alipofika Ubalozini Tanzania, House
Pichani: Bw,Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC akimkaribisha Bibi Lilibeth Asera Tanzania House na alikuwa na furaha ya pekee kutembelea Ubalozi huo.
Meneja wa Miradi Maalum ya mji wa Valejo,California Bibi Lilibeth Defiesta Asera amehimiza kuwepo kwa mahusiano zaidi kati ya miji ya Valejo na Bagamoyo ambayo yatakuwa na tija hasa kwa upande wa Bagamoyo kutokana na ukweli kwamba mahusiano kati ya miji hiyo miwili ni ya zaidi ya miaka kumi sasa. Mahusiano kati ya miji hiyo miwili yaliasisiwa na Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwa na wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Bibi Asera anakumbuka namna Mhe.Rais Kikwete alivyotembelea mji wa Valejo na kupata mapokezi ya aina yake na kuelza kwamba wakati umefika sasa kwa mji wa Bagamoja kueleza "Mahitaji yake Mahususi"ili uongozi wa mji wa Valejo uweze kuyafanyia kazi. Alitaja maeneo hayo kuwa ni katika sekta ya uchumi,elimu,afya na teknolojia ya kisasa. Katika ziara yake hiyo ya Ubalozi wa Tanzania Washington DC, Bibi Asiera alihakikishiwa kufikishiwa ujumbe wake huo kwa uongozi wa mji wa Bagamoyo ili mawasilianzo ya haraka yafanyike.
No comments:
Post a Comment