Wednesday, May 1, 2013

VUA ILIYONYESHA JANA JIJINI DAR YAWATESA WAKAZI WA MBEZI JUU

Gari lenye namba za usajiri T287 AJR, likiwa limetumbukia bondeni jana usiku baada ya kumshinda dereva wa gari hilo, wakati alipokuwa akijaribu kuegesha gari hilo kwa Rivasi na gari hilo kupitiliza baada ya kuruka msingi wa picha ya pili chini na kukaa eneo hilo, mbele ya Baa ya Sensela Mbezi juu kwa Sanya.
Hapa ndipo liliporuka gari hilo na kuelekea bondeni, lakini kwa bahati nzuri dereva wa gari hilo hakuumia wala kujeruhiwa.
Gari hilo likiwa bondeni......
Waenda kwa miguu nao pia wakipata taabu kupanda eneo hili lililovurugwa na magari kwa tope lililotokana na mvua zilizonyesha jijini Dar jana.
Gari hili nalo lilishindwa kupandisha eneo hilo tangu mvua za juzi na kumfanya dereva wa gari hili kuamua kuliacha eneo hili hadi jua litakapowaka.

No comments: