Eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanda likiteketea kwa moto. Eneo liko karibu na bahari. Lilikuwa linamilikwa na serikali na ujenzi chini ya kampuni kutoka Marekani ulikuwa unaendelea. Wazungu wamekusanya baadhi ya vitu vyao na kuondoka eneo hilo.
Spika ameahirishwa bunge hadi kesho kutokana na hali ya Mtwara.
Spika kasema amepokea hali ya vurugu mtwara, hivyo bunge limeahirishwa ili kutoa fursa kwa kamati ya bunge kujadili suala hilo na serikali imetakiwa kutoa majibu katika kikao cha kesho.
Spika kasema kuwa wabunge wangependa kujadili hali ya Mtwara leo lakini watajadili nini wakati hata wao wabunge wamepata taarifa hizo kwenye vyombo vya habari? Hivyo, akaiagiza serikali kuleta majibu sahihi kesho bungeni na kuwaomba wabunge kuwa na subira hadi kesho na kisha akaahirisha bunge. Akahitimisha kwa kusema kamati ya bunge inakwenda kujadili suala hilo sasa…
Barabara ikiwa imefungwa kwa kuweke magogo na mawe.
Mkazi wa Mtwara akinawa uso baada ya kupigwa mabomu ya machozi.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria ya miguu.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria..
Magari ya Watumishi wa Umma yakiungua kwa moto.
Ofisi za Elimu Masasi.
Mitaa kadhaa ikiwa haipitiki baada ya kuchomwa matairi ya gari.
LINDI, Mtwara
Mtu mmoja amefariki dunia kutokana na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara leo, zilizosababishwa na makundi ya vijana kuchoma moto, majengo ya ofisi za umma, nyumba za watu na kufunga barabara.
Hali hiyo imetokana na hotuba ya Waziri wa Nishati Prof. Sospeter Muhongo akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar wakati kauli mbiu ya Wananchi wa Mtwara ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"
Wananchi walalamikia kituo cha Television na Radio TBC kuzuia na kukata mawimbi yake kutoonekana wala kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa muda.
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam wakati Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara wakacharuka!
Kufuatia tukio hilo Daraja la Mikindani limevunjwa na wananchi wenye hasira pamoja na kuchoma moto Jengo la Ofisi ya CCM saba saba.
Nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia yachomwa moto.
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwa ajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.
Kutokana na hali hiyo watu walikimbia ovyo mitaani na watoto wamefungiwa mashuleni huku walimu walimu pia wakikimbia kutoka katika vituo vyao vya kazi.
Katika maeneo ya Magomeni-Mtwara milio ya irsasi na mabomu ya machozi ndio ilikuwa imetawala na kusababisha hofu kubwa.
Kutokana na hali hiyo huduma zote za kijamii zimefungwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
No comments:
Post a Comment