ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 19, 2013

HATIMAYE KANUMBA MPYA AZALIWA PITIA HII HABARI

Lulu akiwa amembeba Kanumba jnr 
Mama Lulu na mama wa marehemu Steven Kanumba wanaonekana kuwa karibu sana siku hizi na hivyo watu kuzidi kuamini kuwa hawana tofauti tena na kusahau yaliyopita. Dada wa marehemu Steven Kanumba amejifungua hivi karibuni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mtoto huyo kupewa jina la Steven Kanumba Jr huku mama mzazi wa Elizabeth Michael(Lulu) na mama Kanumba wakiwa na furaha sana, Lulu pia alionyesha furaha yake kwa kuzaliwa mtoto huyo kama picha zinavyoonekana hapo chini. Tunawapongeza tena na tena wazazi hao kwa kuwadhihirishia wanajamii kwa mara nyingine kuwa kila mtu ana amani na mwenzake na hakuna tofauti yoyote kati yao. Mtoto huyo amepewa jina la Kanumba kama ishara ya kumuenzi muigizaji Steven Kanumba aliyekuwa maarufu Afrika mashariki na kuanza kujulikana kimataifa. Angalia picha........... 

Sura zikiwa na Furaha 
Mama Lulu, Lulu Na Mama Kanumba kwenye picha ya pamoja, Habari kutoka Tanzaniaone blog.

2 comments:

Anonymous said...

kwani kweli mtoto huyo ni wa kanumba au tunataka kuzaa magazeti na kujipatia umarufu? chunguzeni sana wadau wenzangu na mtakuja kujua kwamba mtoto huyu si wa kanumba ni wa pedajee mmoja aliyenona serikalini

Anonymous said...

Ndugu Anonymous! UWE UNASOMAGA HABARI KABLA YA KUKURUPUKA KUKOMENTI! Ona sasa wakati wewe unahoji kama kweli mtoto ni wa Kanumba, habari imesema "DADA WA STEPHEN KANUMBA KAJIFUNGUA MTOTO ...!" Pole Anonymous kwa aibu hiyo. Bahati yako Anonymous mko wengi mno msiotaka tuwajue!!!!