 |
Marehemu Jerome Mpefo
Jioni ya leo katika ukumbi wa Lutheran Memorial, Houston Jumuiya ya Watanzania imefanya harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa marehemu Jerome Mpefo. Harambee hiyo iliyohudhuriwa na Wanajumuiya wengi iliendeshwa vyema kwa ushirikiano wa kaka Domino na James Shemdoe wakisindikizwa na Dj Jimmy. Pesa taslimu zilichangwa pamoja na vitu mbalimbali vilivyotolewa na wanajumuiya kunadiwa ilikuwa ya kufana na ilipitisha lengo lililowekwa la kukusanya $17,000 .Hadi mwisho wa Harambee jumla ya $33,055 zilipatikana na hivyo kuvuka lengo kwa 194%. Mungu awabariki wote waliotoa kwa moyo. Pata picha za matukio katika shughuli hiyo.

|
Kwa picha zaidi bofya read More
12 comments:
Goodbye Jerome .ulikuwa na roho nzuriiiiiiiiiiiiiiii you will be missed
Emmanuel Akili pole sana kwa msiba Huu .
Very nice may GOD bless all the people in HOUSTON you have set a wonderful example. That's what you ushirikiano. May his soul rest in peace. Thank you HOUSTON. Sister from DMV.
I salute you 'll H.TOWN Mungu awaongezee Baraka kwa moyo wenu wa upendo. RIP Jerome.
Kutoa ni moyo si utajiri...Wale wooote mlio jumuika katika Harambee na kumchangia mwenzetu Mungu awabariki sana tena awazidishie pale mlipo toa. Na wale ambao hamkufika Mungu awawezeshe kufika wakati mwingine, na pia bado mnaweza kutoa michango yenu mkawapa familia ya marehemu, isiwe kama kwasababu hukufika baasi huwezi changia, hapana. Kutoa ni moyo-leo kwa mwingine kesho kwako.
Alikuwa ana roho nzuri Jamani u wiiiiii.
huu ndo umoja. Wengine wamekalia magroup too, ukija kwenye usirikiano. zero.
Houston ni mfano wa kuigwa jamani. Hongereni sana kwa kazi nzuri. Mungu awabariki sana. Wafundisheni wa wengine kwamba kutoa ni moyo na sio utajiri. Mwana ametoa na bwana ametwaa. Amen. RIP Bro
Mungu akulaze mahala pema peponi Jarome. Upendo, Upole, heshima, hekima na nidhamu ullyokuwa nayo vinafaa kuwa mfano kwetu sisi tuliobakia. Nimejifunza mengi sana toka kwako. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Amen. Mdau- Washington DC.
I am moving to Houston, nimependa umoja wao hauchagui kabila wala status. bye bye DC.
Mungu akupumzishe kwa AMANI!
Kaka angu sio umoja Watu wameshafariki wengi tu na michangu tuli struggle.Jerome alikuwa ni Mtu wa Watu wewe,sura ya upole,matendo ya upole ,Sauti ya upole,alisaidia Watu.Jerome hakuwa tajiri ila aliwasaidia saana wazazi wake na wadogo Zake na Yaani .Kuishi na Watu vizuri watakukumbuka.Jerome ni loss kwa Watu wa Houston na marafiki ndugu na jamii .utakumbukwa milele jerome
Wewe Uko Houston Lazima uwe Mtu Kama Jerome sio umbea na kutukana Watu .Jerome alikuwa Kama malaika anayetembea duniani ,Yaani usiombe ukutane nae uongee nae.Very humble mke wake mwenyewe kutwaaa alikuwa hamwelewi na hata Kwenye msiba mkewe Ali sema Kwenye speech yake .Huna usafiri kaka wa Watu atamuacha mkewe kitandani kutwaa kusaidia Watu .Mkewe alijitahidi kumbadilisha wapi ?.Ukiahamia Houston uwe mtaratibu.
Post a Comment