Ni mara nyingi tunasikia kuna Watanzania huwa wanarudishwa nyumbani baada ya kufanya makosa mbalimbali kwenye nchi za watu lakini hatujui idadi yao.
Leo tumepata nafasi kwenye exlusive interview kuhusu takwimu kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini South Africa kupitia kwa Second Secretary Habibu Awesi Mohamed.
Anakwambia kila mwezi Ubalozi huwa unawarudisha nyumbani Watanzania hamsini mpaka mia moja.
Wanapokamatwa na polisi, Watanzania hao pamoja na raia wa nchi nyingine hupelekwa kwenye gereza liitwalo LINDELA Johannesburg ambapo hapo ndio Ubalozi huwa unakwenda kuwatambua baada ya kupewa taarifa.
Awesi anasema makosa ambayo wengi wanakutwa nayo ni kama kuishi bila kibali, kwenda Afrika Kusini bila hati za kusafiria, wengine hukamatwa na polisi alafu wanashindwa kujielezea hivyo wanaingizwa kwenye makosa ambayo sio yao.

No comments:
Post a Comment