Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda
Wakati Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda, akiwasili leo kutoka Afrika kusini alikokuwa amelazwa kufuatia tukio la kutekwa, kupigwa, kuteswa na kujeruhiwa, zimefika siku 90, Jeshi la Polisi Nchini halijatoa taarifa za kukamatwa watu waliohusika na unyama huo.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, alivamiwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake, Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam Machi 5, mwaka huu.
Katika tukio hilo, watu hao walimng’oa meno, kumkata kidole, kumjeruhi kwa kitu kizito kichwani na kumharibu jicho la kushoto.
Baada ya tukio hilo, Machi 6 mwaka huu, Kibanda alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na baadaye katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), jijini Dar es Salaam. Baadaye alipelekwa Afrika Kusini na kulazwa katika hospitali ya Mill Park jijini Johannesburg.
Aprili mwaka huu jeshi hilo liliahidi kwamba lingetoa taarifa kwa umma kuhusiana na uchunguzi wa timu iliyoundwa kuchunguza tukio hilo.
Hata hivyo, maofisa waandamizi wa jeshi hilo kila wanapoulizwa wamekuwa wakishindwa kutekeleza ahadi hiyo na kuunyima umma haki ya kujua waliotenda unyama.
Mara kadhaa, Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso, na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu, wamekuwa wakikwepa kulizungumzia suala hilo na kuahidi kuwa taarifa zitatolewa baadaye.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, ambaye ndiye aliyeunda kikosi hicho kila anapoulizwa suala hilo amekuwa akikwepa kulitolea maelezo kwa madai kuwa liko juu ya uwezo wake na kufafanua kuwa lilishapelekwa kwa DCI.
Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote ya maana ya polisi, siyo ya kumatwa kwa yeyote wala kuonyesha walau mwelekeo wa uchunguzi huo, jambo linalotafsiriwa kuwa ni kulipuuza.
Hisia hizi zinatiwa nguvu hata na kauli za viongozi waandamizi wa serikali akiwamo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, bungeni kwamba Kibanda ni nani hadi aumizwe na vyombo vya usalama.
Wasira alitoa maneno hayo yenye ukakasi alipokuwa akijibu hoja mbalimbali kuhusu mjadala wa bajeti ya ofisi ya Rais.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment