Juu na chini ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Umeme Eunice Urio, wakati akimfafanulia kuhusu utendaji kazi wa Mashine ya kufundishia jinsi inavyoweza kuongoza mashine mbalimbali za umeme, wakati Makamu alipotembelea Chuo kipya cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2013.
Juu na chini ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza na kumtazama Mwanafunzi wa umeme, Elia Michael, alipokuwa akielezea jinsi wanafunzi hao wanavyoweza kuunda Sacket ya umeme inayoweza kuongoza mashine mbalimbali za umeme, wakati Makamu alipotembelea katika Chuo kipya cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mwalimu wa Umeme katika Karakana ya mafunzo, Adrian Aloyce, wakati akifafanua jinsi Mashine za 'Automatic System' zinavyoweza kujiendesha zenyewe, wakati Makamu alipotembelea katika Chuo kipya cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2013.
Juu na chini ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbi kumbu mbele ya jengo la Chuo cha VETA, wakati alipotembelea chuo hicho cha Tehama cha VETA Kipawa, leo Juni 1, 2013.
Sehemu ya wanafunzi, walimu wa Chuo hicho waliohudhuria, wakimsikiliza makamu wakati akizungumza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza machache baada ya kutembelea na kujionea Teknolojia ya ufundishiaji inayotumiwa na walimu wa Chuo hicho cha VETA Kipawa.
Picha ya pamoja na walimu na watumishi wa Chuo hicho.Picha na OMR
No comments:
Post a Comment