ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 24, 2013

MAMBO 10 YANAYOSABABISHA MWANAMKE KUSALITI - 9

Kipengele cha sita katika mambo 10 yanayoweza kumfanya mwanamke asaliti penzi, nilieleza wiki iliyopita kuwa ni kitendo cha mwanamke kuhisi yupo kwenye uhusiano wenye sheria na amri. Wanaume wanapaswa kuliangalia hilo kwa makini.

Sheria na amri, humfanya mwanamke ajihisi hayupo huru kwenye uhusiano wake, namna anavyohisi ananyanyasika, humfanya akose raha na msisimko wa mapenzi. Sasa basi, kwa vile anahitaji raha na msisimko, ndipo hujikuta anadondokea kwa mwanaume wa pembeni ambaye atakuwa karibu naye, anayeonesha dalili njema za kimapenzi.

ANAPOHISI MWANAUME WAKE ANAMSALITI
Kuna asilimia fulani ya wanawake hupenda kuishi kwa mashindano na wapenzi wao. Sasa wanapogundua au kuhisi kwamba waume zao wanachagamkia raha za pembeni, nao huamua kutoka ili waende sarasare. Kwa lugha nyingine isomeke ngoma droo.
Wao hufikiri kuwa dawa ya usaliti wa wanaume ni wao nao kutoka nje. Tafsiri hapa ni kuwa kadiri unavyomsaliti mwenzi wako, unakuwa unamuweka kwenye mazingira ya yeye kukusaliti. Atakusababishia maumivu ya moyo, zaidi ya hapo kuna maradhi.
Ipo mifano mingi ya wanawake ambao walikuwa waaminifu sana lakini baadaye wakageuka nyoka na kusaliti baada ya kugundua wenzi wao wanatoka na wapenzi wegine. Mantiki hapa ni kwamba unapaswa kudumisha uaminifu wako ili kumlinda mwenzi wako asikusaliti.
Inawezekana sababu ikawa siyo kukukomoa ili mwende ngoma droo, ukweli ni kwamba watu wameumbwa na kinyaa. Hivyo basi, anapohisi unamsaliti, haraka sana anatumbukiwa nyongo na wewe. Anakosa msisimko juu yako, mwisho kabisa anakuwa hajisikii kabisa kushiriki mapenzi na wewe.
Anapofikia hatua hiyo, anakuwa hana jinsi zaidi ya kupokea ombi la pembeni. Kama wewe hujirusha na wanawake nyakati za usiku, yeye atajipumzisha na kidume aliyemtunuku mchana. Usiku ukirudi nyumbani utamkuta amejaa tele. Kichwani utasema mwanamke wako ni mwaminifu na hana hulka ya kurukaruka.
Utaweza kumbaini mwenzi wako kuwa siyo yule hasa pale utakapokuwa unamhitaji kimapenzi. Hawezi kuwa sawa na yule wa siku zote. Atakuwa anakupa sababu za hapa na pale ilimradi msifanye chochote. Mara nyingine atakukatalia kwa sababu hana msisimko na wewe, kipindi kingine anakuwa amechoshwa na mwanaume wake wa pembeni.
Kuna nyakati atakubali mshiriki tendo lakini hatafurahia. Ataona unampa usumbufu tu kwa maana hajisikii. Kama ilikuwa unamfikisha kileleni ndani ya dakika 20, unaweza kutuama kifuani hata kwa saa mbili na bado atakwambia hawezi kufika juu ya mlima. Ataendelea kukuvumilia lakini mwisho atakwambia ukae kando, maana humpi raha ila karaha.

8. MWANAUME MWENYE GUBU
Huko nyuma katika mfululizo wa makala zangu zilizopita, nimeshawahi kueleza kwamba wanawake hupenda kudekezwa. Hutaka wawe wananyenyekewa, wanabembelezwa na kuongeleshwa kwa kauli laini ambazo huwafanya wajione malkia.
Inapotokea mwanaume anakuwa hodari wa kuzungumza kwa ukali na makaripio, humfanya mwanamke ajione kama yupo kwenye uhusiano usio na amani. Haraka sana, huangalia uhusiano wa wanawake wengine jinsi wanavyoishi na wanaume zao.
Kitendo cha kubaini kuwa mwanaume wake ana kasoro ya kimawasiliano na mwanamke, humfaya atamani kumpata mwanaume ambaye atakuwa tofauti na mwenzi wake. Itaendelea wiki ijayo...

GPL

No comments: