ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 16, 2013

MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI APIGWA NA KUJERUHIWA VIBAYA

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari muda huu amepigwa na kujeruhiwa vibaya damu zinamtoka Puani, amepigwa na vijana wa kisomali, katika eneo la Zaburi kata ya Makuyuni Jimbo la Monduli, Taarifa za awali zinasema baada ya Nassari kuondoka na gari  jingine, waliokuwa wanafuatana naye walienda kujibanza sehemu.

 Kiongozi wa Chadema aliyetambulika kwa jina la Teddy Ndossi na dereva wa Nassari. Dereva wa Nassari Guardian  Palangyo amepigwa mdomoni amevunjwa meno mawili, na kwa sasa wamempiga Katibu wa Chadema wa eneo hilo anayeitwa Kilongola, wapo Kituo cha Polisi Makuyuni kutafuta msaada zaidi.

Jana usiku katika kata ya minepa jimbo la ulanga magharibi vijana wa ccm (green guard) waliwavamia viongozi wa CHADEMA hususani mlinzi wa mgombea udiwani kwa nia ya kutaka kumuua mgombea udiwani wa kata hiyo bw. Maiko, waliojeruhiwa ni m/kiti wa jimbo bw. Kibam Ally Mohammed aliyevaa shati ya draft, katibu wa jimbo bw. Lucas Lihambalimo aliyevaa shati jekundu na bw. Severin Matanila k/mwenezi tawi la Minepa aliyekaa na mwenye bandeji na ni mlinzi wa mgombea.

1 comment:

Anonymous said...

Tanzania imefika hapa? Kama siyo civil war ni nini? Mungu ibariki Tanzania...