ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 25, 2013

MO AWA MTANZANIA WA KWANZA KUTAMBULIKA NA JARIDA LA KIMATAIFA LA FORBES AFRIKA

Mo mjasirimali kijana mwenye mafanikio ya kipekee katika bara la Afrika.

Na Mwandishi Wetu 
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.
Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 30 za kimarekani hadi dola Billioni 1.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.

7 comments:

Anonymous said...

sasa ni kwanini watu wa jimbo lake ni maskini wakutupa? Nafikiri amekuwa mbunge kwenye hilo jimbo kwa kipindi kirefu sana. Kwanini asiwape wananchi wake strategies zakuondokana na umaskini?

Anonymous said...

Huo utajiri sio wa kufanya kazi masaa 100; ni pesa za ufisadi plus za makampuni ya baba yake ambayo walikuwa wanakwepa kulipa kodi. Mwaka 2001 kulikuwa na kesi ya akina DEWJI mahakama ya kisutu ambapo walikuwa wakidaiwa kutoliba kodi kiasi cha mabilioni ya fedha...lakini kesi ikafichwa na waandishi wa habari wakaambiwa wasiandike...
Kwahiyo sio kama ni mchapa kazi sana hakuna lolote ni jasho la wananchi wake...

Anonymous said...

Nasikia jimbo lake limekucha ile mbaya kuna maji na umeme wa kutosha. Sasa jamani mnataka awagawie watu pesa bure ama? Ameleta maendeleo sana pale jimboni mwake ukifananisha na wabunge wengine wanao pigana ngumi bungeni na kutukanana.

Anonymous said...

We mtoa nasaha wa tatu bora umesema umesikia maana ulivyosikia sio sahihi

Anonymous said...

Wewe anon wa 4.04am usitetee upuuzi. Kama hujafika jimboni kwake usizungumze. Inaonekana umeparamia tu kutoa mawazo kwani anon wakwanza amezungumzia kuwapa wananchi wake strategies zakujikomboa kimaisha; wewe unazungumzia kugawa hela. Afterall Dewji huwa anagawa sana hela infact uki-google utaona kuna picha Fulani aliwagawia waalimu pesa. Sisi hapa tunamzungumzia mtu na mafanikio yake ukilinganisha na mafanikio ya jimbo lake havilingani kabisaa. Je ni nini tatizo. Je ni elimu ya watu wa jimbo lake au ni nini hasa. Hayo yakuanza kulinganisha na wabunge wengine hayahusu. Jamani tubadilike uzalendo kwanza tuache kutanguliza siasa kwenye kila kitu.

Anonymous said...

Majungu, wivu, ujuaji na uvivu ndiyo utamaduni wa mtanzania. Kaeni mkipiga kelele na maneno mengi wakati wenzenu wanatengeneza mabilioni ya dola. Unataka awape pesa wananchi wake?

Anonymous said...

We wa mwisho mzembe kupita kiasi