YOHANA MTAKATIFU KUZIPIGA MANZESE
Kwa mara nyingine limeandaliwa pambano la ngumi la ki aina yake ni kati ya mabondia wakimya na wapole usoni na wasiopenda kabisa kuongea Yohana Robert aliekuwa bondia wa taifa na mkongwe katika masumbwi atakapopigana na Yohana Mathayo katika ukumbi wa friends corner manzese siku ya jumapili tarehe 30 mwezi huu.
Pambano hilo linakuwa la kiana yake kwa sababu ya sifa za hao mabondia kuwa ni wacha mungu wazuri kiasi cha yohana Robert kuitwa na wapenzi wa masumbwi “mtakatifu ngumi jiwe” ni mtu mwenye ngumi mojamoja ambazo ni nzito sana na hatari kwa mpinzani nae bondia Yohana Mathayo wapenzi humwita “Tembo mtoto” kutokana na umbo lake kubwa, pia humwita “Yohana mbatizaji” kwani mara nyingi huwaachisha ngumi wapinzani wake kwa kipigo au kubadilisha majina yao, mathayo ana ngumi kali za kuvizia, hutulia muda mrefu na akiachia ngumi moja ikikupata vizuri mchezo umekwisha ni mtaalamu wa kuvizia.
Pambano hili limeandaliwa na mwalimu Hatibu ambae ni mdau
wa karibu wa ngumi na tunaliita pambano la aina yake kwa mabondia wote kufanana majina na matendo na huwa na tabia ya kubeba na kusoma biblia kabla na baada ya pambano ni wapole watulivu lakini ni watu hatari sana ulingoni na lolote laweza tokea wanapocheza.
Pambano hilo ambalo litasimamiwa na PST chini ya Anthony ruta na mapambano ya utangulizi kuratibiwa na Ibrahim kamwe bigright.
Mwalimu Hatibu anaripoti ya kuwa maandalizi yanakwenda vizuri vibali vyote tayari na mabondia watakaowasindikiza kina Yohana na mikataba yao imekwisha kamilika ni Fabian lyimo ambae pambano la mwisho alifanya vizuri Indonesia atazipiga na musa sunga nae Bakari ustadh atazipiga na frank zagarino, wakati huohuo Tasha mjuaji na Rama johncena watatoana jasho.
Pia Yule bingwa wa PST uzito mdogo (minimum weight) goldsilver anaumana vikali na herman Richard. Nae Ibrahim kamwe anathibitisha hilo na linaweza kuwa pambano kali sana la vunja jungu ambalo halijawahi kutokea kutokana na sifa za mabondia hao.
No comments:
Post a Comment