ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 17, 2013

NEW YORK TANZANIANS COMMUNITY SOCCER TEAM

Uongozi wa New York Tanzanians Community unawataarifu wale wote watakaotaka kujiunga na timu yetu mpya ya mpira wa miguu kuwasiliana na msimamizi wa timu hiyo na kocha mchezaji Radyn Nyagaly aka NY Ebra kwa taarifa kamili za mazoezi yanayotarajiwa kuanza rasmi jumapili ya tarehe 23 juni.Timu hii itajumuisha Watanzania wote wanaoishi katika maeneo ambayo Jumuiya yetu inayahudumia na itakuwa ikishiriki katika ligi za Diaspora katika maeneo ya kwetu na bila shaka kitakuwa ni moja ya chombo kitakachopeperusha bendera ya nchi yetu katika maeneo ya New York na vitongoji vya karibu,hivyo basi,Uongozi wetu unasisitiza nidhamu,mshikamano,umoja na udugu katika kuijenga timu yetu.Tanzania Juu, Juu, Juu zaidi.

Msimamizi wa timu/Coach Ny Ebra # 347 475 4313

Hajji Khamis
Mwenyekiti
New York Tanzanian Community.

2 comments:

Anonymous said...

Safi Sana Wana Wa NYC! Tunataka muunde timu yenu muje kukipiga huku DMV then tushuke down south tukawapige bao! Hongereni NYC...maendeleo mazuri.

Anonymous said...

wajibu kupunguza vitambi