ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 3, 2013

SARATANI YA MAPAFU NA DALILI ZAKE



SARATANI au kitaalamu Cancer ni moja ya magonjwa yanayowashambulia binadamu.Kuna aina nyingi ya saratani kama vile ile ya matiti (breast) , mifupa (bones) ubongo (brain), damu (Leokamia) na kadhalika.
Tutazungumzia mfululizo wa magonjwa ya saratani hizo na leo tutajadili saratani ya mapafu, ugonjwa ambao ni hatari sana kwa binadamu.

DALILI YA SARATANI YA MAPAFU
Kuna dalili nyingi za mtu ambaye amekumbwa na ugonjwa huu, moja ya dalili ya wazi ni kupatwa na kikohozi mara kwa mara.
Baadaye mtu huyo ambaye anakohoa atapata tatizo la kushindwa kupumua kwani atakuwa akifanya hivyo kwa taabu sana. Ugonjwa huu usipogundulika mapema husambaa katika tezi ambazo zipo karibu na mapafu hivyo mgonjwa kusikia maumivu makali.
Saratani hii ya mapafu pia inaweza kusambaa mpaka katika tishu nyingine kama vile kwenye ngozi laini ya mapafu na katika moyo hivyo kuzidisha hatari kwa maisha ya mtu anayeugua maradhi haya.
Baadhi ya wagonjwa wa saratani hii ya mapafu huweza kuwasababishia matatizo katika ubongo wao, hivyo kujisikia kuumwa na kichwa.
Maradhi haya baadaye huenda katika ini hivyo kumtia matatizo mgonjwa na kwa hakika hali ikifikia hivyo huwa ni hatari.
Saratani ya mapafu huwa ndiyo chanzo kikuu cha mtu kupatwa na saratani ya mifupa ikienea sehemu zote mwilini.

NINI HUSABABISHA KUUGUA MARADHI HAYA
Zipo sababu nyingi za mtu kuugua saratani ya mapafu lakini uvutaji wa sigara, bangi au dawa za kulevya ni moja ya njia ya kusababisha mtu kuugua maradhi haya japokuwa kuna baadhi ya watu huwa wanarithi ugonjwa huu.

VIPIMO
Vipimo vya kubaini kama mtu ana saratani ya mapafu au la vipo vingi, daktari anaweza kuamua kutumia kipimo kiitwacho kitaalamu CT au kipimo kingine kiitwacho X – rey ambapo mgonjwa atapigwa picha na chombo hicho sehemu ya kifuani.
Uchunguzi huo utaweza kumfanya daktari kugundua kama saratani hiyo ya mapafu ipo katika pafu moja au mapafu yote na ataweza kujua kama mgonjwa ana seli zisizo ndogo au seli ndogo na atajua kama ugonjwa huo umeenea sana mwilini au la!

TIBA
Tiba ya saratani hii hutegemea uchunguzi ambao utagundua ni kwa kiasi gani mtu ameathirika, daktari anaweza kuamua kufanya upasuaji au kwa kutumia mionzi maalum ya kutibu maradhi haya na akigundua kuwa ugonjwa umeenea sehemu mbalimbali za mwili wa mtu anaweza kutumia njia zote kwa mgonjwa mmoja.

USHAURI
Ni vema kila mtu akawa na kawaida ya kupima afya yake kwani magonjwa mengi yanapogundulika mapema katika mwili tiba yake huwa ni rahisi kwa daktari kuutokomeza ugonjwa na pia huwa nafuu kwa mgonjwa kwa kuwa hata gharama ya tiba huwa ni ndogo.
Ni vizuri pia kwa kila familia kujua kama mna historia ya kuwa na saratani ya aina yoyote na unapofanyiwa uchunguzi daktari kumfahamisha jambo hilo kwani kufanya hivyo kutafanya aangalie zaidi.
Ni wazi mtu ambaye familia yake imewahi kutoa mtu aliyeugua saratani ina nafasi kubwa ya kupata ugonjwa huu kuliko mtu ambaye familia yake haijawahi kuugua maradhi haya. Uonapo dalili wahi hospitali.
GPL

3 comments:

Unknown said...

Vipimo hivyo vya saratani hupatikana hospital gani?

Unknown said...

Vipimo hivyo vya saratani hupatikana hospital gani?

Unknown said...

In vema tukawa na kawaida ya kpima afya zetu Mara kwa mara.