ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 15, 2013

SHEREHE YA UWT KWA MAKAMU MWENYEKITI WA PLO NA UJUMBE WAKE

Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akiwalaki Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead na Makamu Mwenyekiti wa POL Tayseer Khalid (mwanaume mwenye miwani) Khalid na ujumbe wake walipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, waliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wanne Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.
Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba (wapili kulia), akiwa na Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO) Jihad Abu Zead akitazama bidhaa za kina mama wa UWT, ujumabe wa Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khali (kulia kwa Jihad), ulipowalisi. Wengine ni Mwenyeji wao, Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migoro na Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
UNAONA WANAVYOWASHANGILIA! Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimwambia Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni, Makamu Mwenyekiti wa PLO, TayseerKhalid na Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Jehad Abu Zead, akimpa kadi mwanachama mpya wa CCM, Mohamed Ali, katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba na Wanne ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wasita niBalozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujaisa
kwa picha zaidi bofya read more
Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akimzadia nguo, Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, wakati cha Palestina (PLO) Jehad Abu Zead, akimpa kadi mwanachama mpya wa CCM, Mohamed Ali, katika sherehe maalum iliyoandaliwa na UWT leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Mamia ya wanachama wapya wa CCM ambao wengi wao ni vijana, wakiwa katika picha ya p0amoja na viongozi baada ya kupewa kadi zao katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Kinamama wakimwayamwaya wakati wa sherehe hiyo
Wengine wakigaragara chini kwa furaha wakati wa sherehe hiyo
Kikundi cha Vijana wa CCM cha Ilala wakionyesha umahiri wao wa kuchgeza sarakasi wakati wa sherehe hiyo
Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi akimwekeza jambo, Mwenyekiti wake, Sophia Simba wakati wa sherehe hiyo
Viongozi wote wa meza kuu wakiwaaga wananchi baada ya sherehe hiyo kufana
Wana-UWT nao wakiwaaga viongozi kwa furaha
Mjumbe wa Kamati Tandaji wa PLO, Jihad akionyesha zawadi aliyopewa na wanachama wa UWT katika sherehe hiyo. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba na Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid
Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba akizungumza wakati wa sherehe hiyo
Jihad akizungumza wakati wa sherehe hiyo
Vijana wanaoshiriki Miss Kanga Party ya Kibaha, wakisalimiana na wageni wa heshima kwenye sherehe hiyo.
Wana-UWT wakiwa wamemzonga Jihad na hivyo Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi kulazimika kutumia msuli kuwazuia, walipokuwa wakimshangilia kiongozi wakati akiondoka Uwanjani
Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba akiagana na Makamu Mwenyekiti wa PLO baada ya sherehe.

PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

1 comment:

Anonymous said...

Sijaelewa kwahiyo hawa wajumbe wa Palestinian nao ni ccm? CCM mnatisha. Kidumu.