ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 26, 2013

SUGU APATA DHAMANA NI BAADA YA KUTIWA ROKAPU KUTOKANA NA KUMWITA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA "MPUMBAVU" MJINI DODOMA.

MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.

Mwandishi wa Habarimpya.com akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.

Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa.

3 comments:

Anonymous said...

Hao ndio wabunge vijana muwatakao jimboni lwake kunatia huzuni sijui kama watamchagua tena na muziki wake ushafade sasa kaka ukipigwa chini na hujasoma utafanyaje? Usitukane wa kubwa zako kiumri na kikazi huo ni ukosefu wa adabu unajichongea wewe mwenyewe kuwa ni mbunge muhuni.

Anonymous said...

Hivi nikisema Obama ni mpumbavu nitapelekwa polisi? Acheni kudumaza demokrasia ninyi serikali ya chama kimoja..ndiyo maana hadi leo nchi inajulikana kama chama kimoja, kuonea watu hasa wanaopinga serikali.

Anonymous said...

Asante wachangia mada hii, Hivi kweli kama kiongozi wa ngazi ya juu, unaweza kutoa kauli ya kuleta machafuko nchini mbele ya bunge lililowekwa kuongoza viongozi na kupanga taratibu za utekelezaji wa majukumu, kauli kama hiyo imtafakari mtoaji kuwa kwenye kundi gani? Tatizo kubwa linaonyesha wazi kabisa bado tuko kwenye siasa ya chama kilekile kimoja! Hebu tafakari majibu aliyotoa mheshimika mkuu wa vyama kwa hawezi kukifuta chama cha kijani! Waachie wananchi watakifuta wenyewe. Sidhani kama kulikuwa na sababu ya kumkamata Mbunge huyu, mbona wasingemkamata Waziri mkuu au kwa sababu amewalenga kuwapa uhuru wa kupiga, Nduguzanguni sheria zifuatwe.Mungu ibariki Tanzania.